Kimenuka: Lady jay Dee afunguka, Atoa wosia wake siku akifa

Yessir, it behooves her to clarify how much she used to pay to each and every member of her earlier "Machozi" band.

Kama aliweza kulalamika kulipwa laki nane kwenye Fiesta miaka lukuki iliyopita, basi atakuwa kwenye nafasi ya kutoa viwango alivyokuwa akiwalipa wanabendi wake wote enzi za Machozi Band na Wanabendi aliyonayo hivi leo...

Aweke wazi ni kiasi gani biashara yake inaingiza kwa mwezi kwa faida baada ya kodi, halafu baada ya hapo aweke wazi ni kiasi gani alivyokuwa anawalipa Wanabendi wake, Wafanya kazi wake enzi hizo na kiasi gani anawalipa wote hawa hivi sasa.
 
Haka Kadada kanaleta unafiki tu......aishie zake
 
Umeongea Ukweli mtupu.... Ila Kipaji hata Kiduchu hana! Kabebwa bebwa pale leo kaachwa Wanabebwa wenzie anapiga makelele Alikuwa na uwezo wa kuimba kumzidi Stara thomas huyo? Akapambane mwenyewe Asitafute huruma za watu.

Kusaga ni kupe
 
Kusaga ni kupe


Mi nadhani hujaelewa post za watu wengi hapa Jamvini.
Watu sio kama tunakataa kuwa Clouds ni wahuni na wanyonyaji.
Sio kama tunawasafisha Clouds.
La hasha, sisi tunapinga unafiki aliouonyesha huyu Malienge.
Wakati wenzake wanalalamika kuwa clouds ni wanyonyaji yeye alikaa kimya.
Hii ni kwa kuwa clouds walikuwa wanapiga nyimbo zake.
Lakini sasa kuna tofauti kati yao ndio anakuja kutuandikia ushuzi wake kisha anawaasa wasanii wawe na umoja...je umoja huo hakuuona mwanzo?

Huo ndo unafiki tunaousema.
So jibu hoja, usije na vioja
 
Dada jde pole saana... ila umenifurahisha sana kwa kauli yako "kila nafsi itayaonja mauti" ..... kwa imani y amo hiyo umenivuta niwe SHABIKI wako


Mjomba usihadaike na rangi ya Ganda...
Ipasue pilipili ndani kisha uionje ndo utaijuwa habari yake.
Huyo hamjui Mungu unaemuabudu wewe.
Asikuvutie kwa maneno matamu kama hayo ile hali yeye alipojihisi ana jini mahaba alimuita Mganga Nyumbani kwake na kisha akashiriki ushirikina ambao nina uhakika Mungu unaemuamini wewe haruhusu ushuzi huo...

Shtuka
 

Heee! Kulikoni?
 
jide Mnafiki.
Na unvyomshauri amtumaini Mungu na ndie atakaemsaidia unajisumbua tu.
Jide anashiriki na mambo ya waganga na ushahidi alishatuonyesha kwenye kipindi chake cha Diary kuwa aliita mganga kwake na akampunga jini mahaba alilokuwa nalo.

hahah Ngoja nijiweke pembeni niangalie mambo yanaendaje
Ila mie napenda Jide ,namtafikia mafanikio siku zote
 
Pole Jide,
jitahidi muyamalize as msamaha ni kitu muhimu tukiwa hapa duniani kabla haujafumba macho.
 
Huyu ni kinega mkomavu. Hii ni Anti virus IV. Hadi msibani wasihudhurie na wala redio yao ya wafu isitangaze kifo chake??? Kusaga tokea amezaa na Zamaradi naona nuksi zinamuandama tu

Eeeeh whhhhaaaattt??_is it true about zama???
 
Pole Jide,
jitahidi muyamalize as msamaha ni kitu muhimu tukiwa hapa duniani kabla haujafumba macho.


KUNA SEHEMU AMEANDIKA MANENO HAYA ...

''Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo
zenu mnazo influence nani apate nani asipate,
na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8
mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili
nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma
na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha
Band yangu''....

HAPO KUNA SEHEMU KASEMA ''tangu niachane na Fiesta mara ya mwisho nilipolipwa laki nane''...KUNA MTU ALIULIZA SWALI LENYE MADINI SANA NDANI YAKE, ALIHOJI JE LAKI NANE HIYO WALIKUBALIANA KUWA NDIO YATAKUWA MALIPO AMA WALIKUBALIANA VINGINE KISHA BAADA YA TAMASHA WAKAMPA HIYO LAKI NANE?

AKAENDELEA KUHOJI NA KUULIZA JE KAMA CLOUDS WALIKIUKA MAKUBALIANO JE NI HATUA GANI ZA KISHERIA ALIZIFUATA?
AU ALITUMBUIZA BILA KUINGIA MKATABA?
AU ALIAMUA TU KUJINYAMAZIA?
NA KAMA ALIAMUA KUNYAMAZA NINI KIMEMPWITA MPAKA AKUMBUSHIE ISHU YA MIAKA KADHAA ILOPITA?

HUO NDO UNAFIKI NA PIA NI MOJA YA NJIA YA KUTAFUTA HURUMA ZA WAZALENDO.
 
Hapa nimekuelewa,
ina maana ugomvi umeanzia kwenye laki nane?
hadi anasema wasiiangalie maiti yake? na laana kibao,
kama kwa kitu kidogo kama hicho anafika huko, je siku akimkuta huyo mume au sijui nani wake amela la na mwingine
itakuwaje, inaonyesha huyu dada ni wa vinyongo na kutaka kulipiza kisasi.

 
Clouds ni genge la wahuni


Huo ni ukweli usiopingika.
Ni kweli kabisa Clouds ni Janga la muziki hapa nchini.
Lakini fahamu kuwa Lady JD ni mnafiki na anajitahidi aseme poo kwa namna ya kujifanya kutoa waraka.
Kuna sehemu wenzie wamemkamata sasa anaona bora akukuruke kwa style hii, na wasioelewa mchezo wameunga mkono ushuzi wake huo.

Kinachomuuma huyo ni kitendo cha baadhi ya wasanii katika bendi yake kutimkia bendi ya Skylight na bendi hii ya skylight kuanza kubamba na kupelekea watu wa muziki kuifananisha Skylight na gari aina ya Range Rover na Machozi Band kufananishwa sawa na Bajaj...

Haya mambo ya kuibiana wasanii kwenye mabendi ni kitu cha kawaida mno katika historia ya Muziki wa dansi hapa nchini.

Hassan Bitchuka alishatimka Sikinde na kutimkia OSS, DEDE juzi kati ametimka Nginde na kutimkia Ndombwa, Maalim Ghulumo alishatimka Nginde na kukimbilia OSS, akina Comandoo, Adam Bakari, Eddy Sheggy nao walishatoka Vijana na kwenda anzisha Njata, achana na hawa akina Banza Stone, Ally Choki, Muumini Mwinyijuma na Hadija Kimobitel...

So kwa watu wa muziki tunatambua ishu kama hiyo hutatuliwa vipi na si kuanza kutafuta huruma za wahafidhina.

Nimshauri tu akasikilize nyimbo kama Chatu ya OSS, Homa imenizidia ya OSS, Mtoto akililia wembe, MV Mapenzi namba mbili, na Talaka rejea za Nginde atapata kujuwa wenzie wakikimbiwa na wanamuziki je huwa wanachukua hatua gani?...
Then mambo yanaendelea.
 
Mnaosema Jide ni mnafiki kwa hoja ya kuwa alikaa kimya wakati wa Sugu mjue kwa mtu mstaarabu yeyote huwezi ukakurupuka bado watu unaongea nao vizuri then unageuka tu kwa sababu wamegomania na Fulani hivi mnafikiri kweli?!! Mana kuna watu mahodari wa kukuchekea wakati uku wana Yao! Sasa mtu uliye na upeo na heshima zako this is how we handle it! Identfy the problem! Keep Calm, take action, na kubwa huwani kukeep distance but Mara nyingi watu wa hivo wataendelea kukufuatilia hapo kila mtu Ana namna ya kubackfire! Hii ni yeye Jide kaona atoe dukuduku lake kwa style hii! Na nadhani kafikiri mbali zaidi mana ni kweli hii ni radio tunaisikiliza sana tukipata msiba wa mtu Kama huyu Jide Hana tofauti na alivokuwa kanumba tunampenda! Watanzania lazima tujivunie vipaji vizuri unique tunavokuwa navo Kama hivi! Clouds watacover msiba wake mwanzo mwisho sasa kaongea Lililo Moyoni mwake kaona mbali! Yani watu waliokua wanakutia simanzi ukiwa hai wawe mstari wa mbele ukifa? Kwa hiliwatu tujifunze kuheshimana! Clouds Kama wanavojiona ni wa muhimu kwa jamii kuna watu ambao wajue jamii inawatambua vile vile so wawape heshima Yao!
 


Then Mamndenyi mfano mie leo hii nikikuzaba kibao, kisha ukiugulie weee then maumivu yakikata tunaendelea kuwa marafiki kama vile hakuna kilichotokea.
kisha miaka ya katikati baadae wanaibuka watu na kutoa malalamiko yao kuwa Gang Chomba ana tabia ya kuwatandika watu makofi, kisha wewe Mamndenyi still unajikausha tu huku unawaona wale wanaolalamika ni kama mazezeta vile.
Then baada ya aka kama 5 kukatika uibuke na kuanza kusema kuna mwaka Gang Chomba alishanitandika kibao.
Ooh nikifa Gang Chomba asije kunizika...
Je wenye akili watakuona umzima kichwani kweli?

Sasa ndio huyu binti aliekimbizwa kanisa la Sabato.
Alipolipwa laki nane akanyamaza na kuendelea kuwa na ushost na hao aliosema wasije kumuaga akifa, miaka kadhaa ilopita wasanii wenzake wakaanzisha harakati za kupinga unyonyaji wa Clouds, then yeye akajikausha tuliii kama Nyau aliefumaniwa, asa sasa hivi anakurupuka na kujishaua eti alilipwa laki 8...

Huu ndo unafiki.
 


Skia...
Anasema jamaa walianza kumchukia mara baada ya yeye Lady JD kukacha show za Fiesta kwani alilipwa laki 8.
Ila ndo hajatuambia kuwa jiwe 8 hizo zilikuwa na mkataba, au alifanya kazi kishkaji bila mkataba, au aliambiwa atapewa 3M Tanzanian shilings then wakampa jiwe 8?

Kama hiyo haitoshi ametuthibitishia kuwa tangu hapo maelewano hayakuwa mazuri na mgomo baridi ulianza...
Sasa ni yeye kwa kukaa kwake kimya ndo kumemfikisha huku alipo sasa.
Kama angeungana na wahanga wenzake kupaza sauti huoni kwamba angeeleweka zaidi?

Mwambie hivi kujiongelesha ongelesha hakupunguzi maumivu ya jino.
Afunge bakuli lake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…