Kimenuka: Lady jay Dee afunguka, Atoa wosia wake siku akifa

Kimenuka: Lady jay Dee afunguka, Atoa wosia wake siku akifa

Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.

Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.

Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.

Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.

Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.

Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.
Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.

Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.

Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.

Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame
Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.

Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai
Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.

Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.

Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..

Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.

Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani??
Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??

Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.

Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma??
Roho gani hiyo??

Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu

JIDE
 
I thnk Jide has a point..

N by the way kwanini walalamikie wao tu??? Alianza Sugu sasa Jide. Na wote hao ni malegend wa mziki wetu.

CLOUDS BADILIKENI

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Huyu naye anachosha kwani Radio ni Clouds tuuuuuu au anataka attention..Radio zipo kama utitiri bongo shida ipo wapi? Judith Wambura umezidi na wewe kha! Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza hujawahi sikia msemo huo..Eti wosia nikifa kabla ya fudenge na fudenge basi bla bla bla...ili mradi tu.
 
Safi sana JIDE useme ukweli mapema sababu ukifa akina ruge ndo watafurahi umetangulia na watapiga nyimbo zako kutwa nzima ila kama umeshaacha wosia hakuna kitaharibika coz hao clauds wanajidai wao ndo industry ya mastaa nakuaminia komando jide naamini utafika mbali bila msaada wao na watabaki wakikaa vikao visivyo na mwisho VIVA JIDE
 
Huyu naye anachosha kwani Radio ni Clouds tuuuuuu au anataka attention..Radio zipo kama utitiri bongo shida ipo wapi? Judith Wambura umezidi na wewe kha! Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza hujawahi sikia msemo huo..Eti wosia nikifa kabla ya fudenge na fudenge basi bla bla bla...ili mradi tu.

Pakawa hujaelewa au wewe ndo Ruge coz hata antivirus walishapambana sana na hao clauds tatizo nin?
 
Last edited by a moderator:
mekuelewa JIDE kama hunipendi nikiwa hai basi usinipende nikifa..........
 
Ufuatao ni wosia wa mwanamuziki Lady JayDee, ambapo baadhi ya matakwa yake ni kwa Clouds FM kutopiga muziki wake, na mapedejhee wa kampuni hiyo, Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba wasihurudhie msiba wake.

“Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.

Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.
Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.
Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.

Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.
Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.

Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.
Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.

Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.

Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige mawe. Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.

Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai. Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.

Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.

Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.

Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.

Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..

Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.

Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani?? Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??
Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.
Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma?? Roho gani hiyo??
Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu”

JIDE
 
Mmmh, huyu ni Judith Wambura kweli, kama ni kweli basi amefunguka....ni vizuri kuambiana ukweli daima,watu wengine huogopa kusema ukweli sababu ya woga hata hivyo wakumbuke kuwa 'HAKUNA DHAMBI KUBWA KULIKO ZOTE KAMA WOGA'.

Brother Ruge na Kusaga if at all you have been doing these things, it's high time now you change immediately. wasanii watawakimbia wote, jaribuni kuwa SMART na NIDHAMU. Such a coincidence JD anawalalamikia naona hata SUGU amewahi kulalamika, infact niliwahi kujiuliza why,,,,,,,,,,,aliacha kazi kwenu na sasa anasikika TIMES FM, isije kuwa ni kwa sababu ni mume.

Judith kama kweli ni wewe uliyeandika haya na kweli iko ndani ya haya uliyoandika, simama hivyohivyo MUNGU yuko upande wako kama alivyo upande wa SUGU.

MUZIKI NI USHINDANI SI UADUI
 
Ndugu zangu wapendwa kwanza napenda kmshukuru Mungu mwenyezi Muumba mbingu na nchi mjaza neema ndogondogo na kubwa nene na fupi kwa kutupa siku nyingine tena kama hii kumshukuru na kumtukuza;;;;;;;;Ndugu zangu watajwa hapo juu kaka zangu ruge na joseph sipendi kuongelea mengi yalioandikwa mitandaon ila ni wakati wa siku za mwisho kutengeneza maisha yetu;;aijalishi mlitendeana mnatendea ubaya gani lakini asb hii ya leo nimewiwa kutoa wazo langu kama mtumishi wa bwana
 
Umenifurahisha sana Jide, kusaga na ruge ni madhalimu wakubwa
 
Mpendane msaidiane mrudishe mapenzi yenu kama kaka na dada msiwape nafasi shetan kusikia malumbano lkwenye vyombo vya habari;magazetin na mitandaon wewe kaka na dada tuzidikuwaombe hili Mungua arudishe upendo wa agape waliokuwa nao zamani kama kaka na dada
 
Mungu wa mbinguni inusuru nchiyetu mbona kuna fukuto kila mahali?tusameheane jamani,moyo urudi moyo usamehe,kanisa lahitajika hapa kufanya uponyaji.
 
Jide mdogo wangu pole sana hawa jamaa ni washenzi sana lakini ipo siku kibao kitageuka na wao zama zao zitaisha.
 
Well you sayed! Or well said?,there's no such English word in English dictionary, hiki kingereza jaman tutumie lugha yetu tu, tutaeleweka vizuri.
 
Back
Top Bottom