Kimenuka: Lady jay Dee afunguka, Atoa wosia wake siku akifa

Kimenuka: Lady jay Dee afunguka, Atoa wosia wake siku akifa

Au ndo sababu ya,
sababu ya.....

Hili joto la hasira ambaa... Naruka Mwenyewe..
 
Katika hao wawili naskia mmoja wao akiona tu msanii wa kike chipukizi zipu inagoma kufunga hadi ammwagie mbegu ....
 
Jide mdogo wangu pole sana hawa jamaa ni washenzi sana lakini ipo siku kibao kitageuka na wao zama zao zitaisha.


Mkuu Ritz; Hawa ni mabeberu kama mabeberu wengine. Wamiliki wa vyombo vya habari ni wanyonyaji wakubwa kwa wasanii wetu( kumbuka yaliyowakuta akina masanja na wenzake kidogo hata majina yao ya kisanii wapokonywe). Ile siku nilivyoona walilia TCCRA isifunge mitambo ya digitali kwa maslahi ya walalahoi nilishangaa sana, mambo yao yakigoma wanasema kua wanawatetea walalahoi lakini hao hao wananyonya vijana wa walalahoi!
 
Damn! What the flip is going on between her and them?

So far I've seen shots being fired from one side only and the other side is not returning any fire (at least not publicly).

Just wondering why is she so mad. What exactly did they do to her to make her this mad?

Thought you knew better man! Seriously something sinister is going down. Joe bhana kwa nini lakini?
 
Wamemzibiaje lakini? Na kuna ushahidi gani kwamba wamemzibia? Na kwani Clouds wao ndo wamiliki na wahodhi wa riziki zote za burudani Tanzania nzima hadi kuweza kumzibia msanii kama yeye au hata mwingine?

Nyani hawajamaa wana influence hadi wadhamini!! Brother hawa jamaa wasikie tu! Hawa ni mafia wa entertainment industries!!!
 
Ant virus version 3 comming soon................................
 
sugu na magenge walionekana wahuni sasa KOMANDO naye kaingia vitani
 

Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.

Katika kipindi hichi ulipoamua kukaa kimya ulizigharimu harakati nyingi sana.....

Kifo cha Gangwe Mob baada ya wao pia kugomea mkataba wa Smooth Vibes, harakati za awali za Hiphop Summit na agenda zake, harakati za kikosi cha mizinga, harakati mpya za vinega....... Bado ulikuwa juu tu.

Lakini hujachelewa labda vita hii uliyoianzisha itasisimua na kuamsha mapambano makubwa zaidi kuwaangusha hawa mbwa kwamba hatuwakatazi kufanya biashara ila WATUACHIE MUSIC YETU!!

Nadhani mnakumbuka hata William Wallace katika Braveheart wakati wenzake wapo busy na mapambano ya kudai uhuru ye hakutaka kabisa kusikia hizo habari na alikuwa busy na mapenzi tu ila siku alipoonja machungu ya ukoloni huo kwa kuuawa kwa kipenzi chake, alianzisha vita yake ambayo ilikuwa kubwa kuliko zilizotangulia.

Karibu Jide kwenye mapambano yaliyopoa, ambapo kila aliyejaribu kupambana alionekana ni mlalamishi na mkorofi mbaya zaidi na kundi kubwa la wasanii masikini wasio na akili na wachumia tumbo wanaotoka uswazi.

Karibu sana.
 
WOSIA WANGU KAMA IKITOKEA NIMETANGULIA KUFA KABLA YA RUGE AU JOE KUSAGA

762500885.jpg


Wsafi sanaaaa maana dunia ya sasa kikaa kimya ni ugonjwaaaa
 
COMANDOOO, COMANDOO, BIG UUUp, Umewavua nguo hao jamaa, na hako karedio kao ka Chama. Chezea Mura+Mangi weye.
 
Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.

Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.

Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.

Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.

Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.

Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.
Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.

Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.

Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.

Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame
Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.

Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai
Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.

Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.

Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..

Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.

Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani??
Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??

Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.

Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma??
Roho gani hiyo??

Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu



Source :ladyjaydee.blogspot.com
 
Wamemzibiaje lakini? Na kuna ushahidi gani kwamba wamemzibia? Na kwani Clouds wao ndo wamiliki na wahodhi wa riziki zote za burudani Tanzania nzima hadi kuweza kumzibia msanii kama yeye au hata mwingine?

Au nawe ni mmoja wao nini?kwani malalamiko yao ndo umeanza kuyasikia leo kwa Jide peke yake?
May God protect you J wasije kuchinjia mbali wakati bado twakuhitaji. :angry:
 
Hii makitu naona imekuwa ya upande mmoja tu ni mtu mmoja analaumu upande wa pili.Ngoja ifike siku tutasikia ya upande wa pili tutachanganua. Nadhani ndiyo njia sahihi ya kusuluhisha jambo. Hata katika matembele kuna baadhi vinaliwa na vingine hutupwa kule. Nimepita tu jamani maana panapofuka moshi .......

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom