Prof ujue huu ujinga wa wanawake kutumiwa insta na kwenye mitandaoni mingine umeanza taratibu na Sasa unajua kwa Kasi ya ajabu.
Walianza kwa kumtusi Hamisa, kisha zari Sasa Kendra nakuambia kesho itakuwa ni zamu ya mwanamke mwingine.
Kipindi cha nyuma wema alitusiwa sana akina Irine na wengine.
Cha ajabu hakuna mwanamke yyte aliyesimama kusema jambo hili halikubaliki yaan wanawake nao tukawa ni sehem ya kutoa matusi hayo pasi kujali kwamba wanawake hawa hawana tofauti na wasiokuwa mastaa.
Haya matusi ya nguoni ambayo tunaruhusu hawa vijana wadogo wa kiume watutukane ni kwasabb wanajua wanawake hatupendani na hivyo hakuna atakaye simamia kulipinga hili.
Hivi wanawake wakipaza sauti unafkir hata kuna mtu angenyua simu yake na kuandi ka upuuzi huu?
Cha ajabu kabsa huyo aliyempost Kendra na huyo shamte kutumiwa hizo picha ba mwanamke. Yaani nkajiuliza hivi ni uzuz wa kiasi Gani huu? Yaan mtu unamfuatilia mwanamke mwenzio ili umpige picha kumdhalilisha kwenye mitandao?
Nakuambia ukombozi wa mwanamke hauwez kufika ikiwa Hali ya chuki miongoni mwa wanawake haijaondoka.
I feel so sad kwa wahanga wote wa huu udhalilishaj kuanzia hamisa, zari na Kendra
Sent using
Jamii Forums mobile app