Kimenuka P-Funky Majani na Jose Chameleon, kisa wimbo wa 'Bomboclat'

P funky endelea kukaza upate haki yako mzeee
 
Umeleta angle ya mwajiriwa na mwajiri ambapo hakimiliki mara nyingi huwa ya mwajiri. Hata kati ya mwajiri na mwajiriwa haimaanishi kwamba hati miliki itakuwa ya mwajiri wakati wote-suala linaloangaliwa ni je mwajiriwa alitegemewa kutengeneza kazi ya IP katika majukumu yake ya kila siku? Kama hakutegemewa, haki ya umiliki ni yake na sio ya mwajiri.

Bottom line, anayetunga kitu chochote ndiye mwenye haki ya umiliki. Lengo la sheria ya hakimiliki ni kulinda kazi ambayo mtu ametumia akili na ujuzi wake kuifanya. Hivyo kama umeajiriwa na una akili, ukitengeneza kazi ambayo ni extraodinary lazima uombe consideration ktk kazi hiyo bila kujali mlikubaliana kitu gan kwenye mkataba. Producer anayejitambua, hata kama ameajiriwa atahakikisha ana haki ya asilimia fulani ya umiliki katika beat anazotengeneza.
 
Sheria ya hakimiliki inaanza kulinda kazi yako mara tu unapokuwa umeikamilisha/maliza. Haihitaji registration kama Patents and the like. So kutoandikishana mkataba wa umiliki hakumnyimi haki ya umiliki mtunzi wa beat.
 
Very complicated.
If it was complicated DW would not be seeking to settle out of court. Even Chameleone's tone does not suggest he claims ownership-he just says he was paid peanuts!
 
Duh!!! Eti anayetunga kitu chochote ndie mwenye haki miliki... ni sheria ya wapi hiyo?! By the way, kwanini aombe consideration wakati umeshasema creator ndie mwenye haki miliki? Hayo mambo ya kuhakikisha ana asilimia fulani hana haki miliki na ndio maana nikasema, prior to contract, lazima Producer aweke terms za kuangalia anapata nini na nini kwenye kazi zake lakini haimaanishi kwamba yeye ndo mwenye haki miliki! Na ndio maana nikakupa mfano wa screenwriter... anaandika script akiwa peke yake nyumbani huku akitumia kila kitu cha kwake! Lakini akishauza tu, anakuwa ame-transfer copyright ownership lakini kama anafahamu, ata-demand pamoja na lump sum payment, lazima awe na haki (sio haki miliki) ya ABC kv royalty, bonus, t-shirts sales n.k!!!!!

Kwamba, nimeleta habari za mwajiri na mwajiriwa labda kama hukunisoma vizuri! Inapotokea total sales, hiyo inakuwa considered as Work For Hire.
 
If it was complicated DW would not be seeking to settle out of court. Even Chameleone's tone does not suggest he claims ownership-he just says he was paid peanuts!
Hiyo complicated nimezungumzia general contract issues na ndio maana watu wengi wanapoteza haki zao! Issue ya P Funk nimeshaweka wazi kwamba kwa jinsi industry yetu ilivyo lazima atakuwa ndo mwenye exclusive right.

Kwamba kama ni complicated mbona Walt & Destiny wanataka ku-settle nje ya mahakama haimaanishi kwamba hivyo unavyodhani wewe! Walt & Disney ni wafanyabiashara na tangu ile filamu iingie sokoni ni takribani miezi 3 hivi sasa! Kutokana na hilo, hawawezi ku-jeopardize flow of business kwa kupelekana mahakamani cuz' inaweza kuja court injunction kwamba any business related na filamu husika isimame hadi pale issue itakapokuwa settled! Na itoshe tu kusema kwamba, business entities nyingi US zinapendelea kumalizana nje ya mahakama kuliko kinyume chake!
 
Duh!!! Eti anayetunga kitu chochote ndie mwenye haki miliki....
That is the spirit of the law. Wewe unaijua sheria ya hakimiliki lakini hujui madhumuni yake. Pia prior contract does not matter, sio fair ukajifunga na mkataba uliosaini miaka 10 iliyopita ukashindwa kufaid matunda ya ubunifu wako. Kama wewe ni mwanasheria, jua unawaangamiza wateja wako ambao ni watunzi kwa sababu ya kukariri lecture notes. Nenda na spirit of the law. Hakuna mtu ana haki ya kufaidi matunda ya akili ya mtu mwingine, kazi ya kutunga ni tofauti na kubeba zege.
 
Sheria ya hakimiliki inaanza kulinda kazi yako mara tu unapokuwa umeikamilisha/maliza. Haihitaji registration kama Patents and the like. So kutoandikishana mkataba wa umiliki hakumnyimi haki ya umiliki mtunzi wa beat.
Sheria ya wapi hiyo?! Kwamba, kwa mfano mimi nimeandika screenplay na nimekuuzia wewe! Hapo bado copyright inabaki kwangu kwa sababu tu ndie mwandishi?
 
Kumbe unazungumzia vile ambavyo ingepaswa kuwa... kwamba hakuna mtu anayepaswa kufaidi matunda ya akili ya mtu mwingine!!! By the way, anafaidi matunda yako kivipi wakati umeshalipwa kutokana na creativity yako?
 
Kumbe unazungumzia vile ambavyo ingepaswa kuwa... kwamba hakuna mtu anayepaswa kufaidi matunda ya akili ya mtu mwingine!!! By the way, anafaidi matunda yako kivipi wakati umeshalipwa kutokana na creativity yako?
Creativity is priceless! You cannot buy it. How much would you pay a person who created Monalisa art!? My point is, an employed creator should understand that he/she cannot be paid adequately for his/her work through salaries. Never! With this in their mind, they can negotiate better contracts before initial contracts and after.
 
Kwanini wa-negotiate wakati umeshasema copyright ni za kwao?! Ukisema wa-negotiate ni kwamba unakubaliana na mimi ingawaje umenipinga?!

That's one, but two, waki-negotiate, creator atakachopata ni RIGHTS associated to his/her work but not COPYRIGHT! Hapa tusichanganye kati ya Haki na Haki Miliki!

Suala la Copyright kubaki kwake litatokana na hiyo negotiation kwamba, creator anauza ABC but NOT COPYRIGHT lakini si kwamba hii copyright inabaki kwake by default. Kitu ambacho non-negotiable ni CREDIT.
 
Huu ufafanuzi wako nimeupenda sana, na ndio mfumo anaotumia Hermy B wa "B hits" kwenye kazi zake. Chanzo cha ugomvi wa Hermy B na AY na Mwana FA ni mfumo wa miliki ya midundo (beats), ambapo kwenye kila production ya beat jamaa lazima awe na percent yake kama producer. Hili nadhani halikuwapendeza vijana hawa, kiasi kwamba wakahisi kama wanaonewa. Nilimsikia mwenyewe Hermy B akihojiwa na Clouds radio kipindi cha XXL kuhusu mfumo huo wa umiliki wa midundo, kwamba huwa hatoi exclusive rights kwa wasanii kuwa wamiliki wa beats, ila yeye ndio anamiliki beats na kisha kuwapa vijana wake kuweka vocals na manjonjo mengine. Kwenye kila matumizi ya hiyo beat, iwe matangazo ya biashara ama vinginevyo, lazima naye apate mgao wake kama original creator wa hio kazi. Ni mfumo complex kiasi chake, ambao haueleweki kwa producers wengi wa Kitanzania.
 
Good... I love this. Producers wengi wanaofuata hiyo model, yupo heri beat akupe FREE of charge lakini copyright inabaki kwake na yeye ndie anakuwa na exclusive right huku artist akibaki na non-exclusive right. Atakachofanya producer ni kuandikishiana mkataba na muhusika unaoorodhesha nini anakitoa na nini atapata but ALWAYS, atakachotoa hakiwezi kuwa Copyright!

Na kama ulivyosema, ni mfumo ambao ni very complex na sio kwenye muziki tu bali hata kwenye filamu. Na ndio maana kwa wenzetu, wanatumia Wanasheria wanaoifahamu vyema entertainment industry na hawa wapo licensed as Entertainment Attorney na sio kwa sababu tu una LLB ndio unaweza kushughulikia mikataba ya aina hii!!!
 

Hili ni kwa walioajiriwa tu! Kama mtu amejiajiri kama PFunk hahitaji kunegotiate na yeyote kuhusiana na beats.
 
Umegonga nyundo ndg. Sio kila mwanasheria ana uwezo wa ku deal na kila suala la kisheria, ndio sababu kuna specialization kama vile criminal, tort, contracts, commercial nk. Nadhani wanasheria wa kazi za muziki na filamu ni wachache sana kwa hapa kwetu.
 
Hili ni kwa walioajiriwa tu! Kama mtu amejiajiri kama PFunk hahitaji kunegotiate na yeyote kuhusiana na beats.
The problem una-generalize mambo!!!! Ngoja nikuulize: Assume mtu wa Walt & Disney alimu-approach Majani moja kwa moja lakini walifanya hivyo baada ya kuwa wameusikia mahali wimbo uliotumia hiyo beat!

Je, unataka kuniambia kwavile tu wamesikia au Majani amewaambia yeye ndo katengeneza hiyo beat hapo hapo Walt & Disney wangefanya biashara na Majani bila kujiridhisha kwamba yeye ndie copyright owner?!
 
Hapa kwetu hao watu ni wachache sana na sidhani kama wapo ambao wamejikita kwenye hilo suala. Ndo vile tu, mtu unakuwa na copyright issue na hakuna specialized entertainment attorneys basi unaamu kwenda kwa yeyote ambae ana abc ya tasnia ya burudani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…