Kimenuka P-Funky Majani na Jose Chameleon, kisa wimbo wa 'Bomboclat'

Kimenuka P-Funky Majani na Jose Chameleon, kisa wimbo wa 'Bomboclat'

Kama chameleon amepewa dola 50,000 je faida ya hiyo filamu ikiingia sokoni itakuwa ngapi? jumlisha na gharama ku-shoot USA.
Ndio mimi jibu langu ni kuwa unahisi walt Disney hawwezi lulipa usd 50000 kwani watapata hasara. Kwa taarifa tu gharama za maandalizi tu ilikuwa zaidi ya dola millioni moja na nusu
Bajeti ya hiyo filamu ni dola million 14.
 
Kwani beat hiyo chameleon hakumlipa majani wakati ana mtengenezea huo wimbo? Nadhani wimbo na beat ni mali ya msanii sio vya producer, bila hivyo basi producer itabidi alipwe kila msanii anapoingiza hela kupitia wimbo na hiyo beat. P funk ilifaa awe analipwa kwa kila show ambayo chameleon ameumia huo wimbo na beat, mauzo ya cd, iTunes, ring tones nk.
Nope, beat always ni ya producer. Ndiye anayetunga hiyo beat na haki ya umiliki wa producer inalindwa na copyright laws. Ni kama wewe ununue software mfano Windows 10, una haki ya kuitumia lakini sio kuuza wala kumpatia bure mtu mwingine maana kwa kununua hiyo CD umenunua haki ya kuitumia na sio umeuziwa umiliki. Hili jambo maproducer wengi ambao hawajaenda shule hawalitambui-wanawaachia beat wasanii ndo wafaidike.

So hata kama Chameleone angelipia hiyo beat ili itumike kwenye bongoclat, bado PFunk ana haki na hiyo beat kama beat itatumika kutengeneza wimbo mwingine au kama itatumika kama soundtrack.

Kwa kifupi, sheria ya hakimiliki hairuhusu yafuatayo:
-kunukuu
-kubadilisha(modify)
-kutumia kwenye maonyesho
-kutafsiri
-kuiga
-...
Hii ni kwa kazi yoyote ya kisanii-wimbo,movie,beat,mchoro,program za computer,nk.
 
Jose kafanya utapeli wa hali ya juu halafu ukifuatilia maelezo unaona anachulia poa tu. Wajameni uhuni kwenye kazi haufai
 
Cha kujiuliza Je majani aliregister hyo beat tangu mwanzo ili kusecure copyright protection?
 
Hapo P Funk akikaa anapata hela ya kununua hata Land Cruiser Amazon used.
Bado ni hela ndogo sana! Pharalle Willium Aliiba nae kazi za watu akaambiwa alipe ($ 7.3 Mil) (£ 4.8 Mil) sema P Funk akiwapata wanasheria wazuri anauaga umaskini!

Unakumbuka ishu ya Mwana Fa na tigo sijui ilikuja kuishia wapi!! Sheria za kulinda maslai ya kazi za wasanii sehemu kama Marekani ni kali sana
 
sasa namuamini shigongo alivyolalamika kutapeliwa na Camelion, bahati mbaya wabongo wengi wakabaki kumtupia matusi shigongo eti kisa cameleon ana pesa hawezi kudhulumu, haya sasa wayaone na ya huyu.
 
Komaa p funk huuo jose ni tapeli huyo
Na ukikomaa hapo unakula hela ya kutosha tu
 
Back
Top Bottom