Kimeumana! Gambo amshukia kama mwewe mkurugenzi wa jiji la Arusha

[emoji13][emoji13][emoji13]Ana nguvu gani Gambo wewe?? Chuki tu na uzushi. Huyu kila KIONGOZI hamtaki, amesahau hata huyo mkurugenzi alimpambania mpaka akawa hapo alipo[emoji13][emoji13], Ana nguvu yoyote kuzidi chama na serkali. Na assipojirekebisha ni one term mp, kamweleze. Nakwambia haya nikiwa kada kindakindakinwa CCM na mwananchi mbobevu wa Arusha na vitongoji vyake vyote. Yani mi Mzee wa chuga, mweleze huyo kijana atulie afanye KAZI, aache migongani na viongozi wenzake. Akae vizuri na Mongela, na Sophia hata na mkurugenzi. Mwambien taratibu akuelewe
 
Kwani Gambo aluchaguliwa na wananchi au kikosi maalum kiliiba kura kwa manufaa ya Ccm??
Mbunge wetu wa rohoni ni Lema..
 
Laana ya uporaji inawatafuna
 
😳🀣🀣

Kwa hiyo Gambo ni mwepesi Sana kisiasa?!!
 
Ugonvi wa ndugu ngoja nichukue jembe nikalime
 

gambo hajachaguliwa Arusha, alipachikwa tena ilikuwa alimanusura kuanzia kura za maoni ndani ya chama na mwishowe uchaguzi najisi 2020.
Asitake kujitutumua, kwanza ndio sura ya mwisho
 
Gambo anaanza kulikoroga baada ya kukorogewa. Hii tabia ya viongozi kukorogana hadharani ... Wajitafakari
 
Hakuna sehemu inasema mbunge lazima ualikwe kwenye huo mkutano, na wewe itisha wa kwako uongee na wananchi sio kulalalmika na kutoa mitusi isiyo na tija, halafu hata ubunge hukushinda mliiba kura wapuuzi nyie
 
Siasa ni kama ukichaa. Unatafuta ubaya kwa mbaya wako Siku zote kutengeneza Uzuri wako
 
Hivi hapo Arusha kuna nini mbona kama viongozi wote huwa wanavurugana tu! Au ni kile kidude cha Meru?
 
Gambo akae Kwa kutulia Ili apakatwe vizuri,yeye kipindi akiwa RC hapo alikua anamfanyia figisu Lema Leo analia Lia nini hapo?
Tena natamani huyo mkurugenzi abaki hapo mpaka 2025 uchaguzini tuone huyo kiherehere atabebwa Kwa mbeleko ya mkurugenzi Gani?

Shwain!
 
Uongo ni kipaji. Alichaguliwa na wananchi gani? Yeye alipokuwa RC mbona alitesa watu vibaya sana? Mbona aliwanyanyasa walio chini yake kwa kigezo cha yeye kuwasiliana na Rais moja kwa moja? Mbona aliweka checkpoint ili kuwajua wanaoenda kuwasilimia alioshiriki kuwaweka rumande? kwenye uongozi wake watu wameumizwa sana. Anyamaze tu. Malipo ni hapa hapa duniani.
 
Wananchi gani waliomchagua Gambo,?aache ujinga,aliyempachika hapo alishakufa kitambo,alichokuwa anamfanyia Lema kinamrudia atulie anyolewe
 
Kwa hiyo alikuwa anamchamba Mkurugenzi?😝😝😝😝😝
 
cc:mrishomgambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…