Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 37,333
- 50,241
Gharama za ushuru anazilipa mlaji/ mtumiaji wa mwisho.Baada ya Trump kupandisha ushuru kwa bidhaa za mataifa mbalimbali duniani ikiwemo China sasa Wamarekani wameanza kujionea kupanda kwa gharama za bidhaa.
Amazon moja ya wauzaji wakubwa wa bidhaa za kutoka China wamekuja na hii idea ili wajisafishe mbele ya wateja wao wasionekane wabaya lakini baadhi ya wachambuzi wanasema ni kama kupandikiza chuki kwa utawala wa Trump.
Amazon wamesema kwenye kila bidhaa wataonyesha bei ya bidhaa na kiasi kilichoongezeka kwenye bei hiyo kutokana na ushuru uliongezwa na utawala wa Trump.
Msemaji wa White House amekuja kwa kasi mwendo wa Ngiri mkia juu kinyeo nje na kuishutumu Amazon kuwa "Hiki ni kitendo cha chuki na kisiasa cha Amazon."
Sijajua kosa la Amazon ni lipi? Kusema ukweli kunawafanya Amazon waonekane wana chuki na utawala wa Trump.
China is winning by not doing anything and simply waiting. Trump master tariff war is exploding in his face. The game is the game.