Kimeumana Vanilla Njombe: Ni utapeli mtupu

Baraka21

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2021
Posts
1,262
Reaction score
3,184
Ujumbe wa DC Njombe kissagwakisakasongwa kuhusu VanillaNjombe

📍Serikali bado inafanyia kazi maswali mengi yaliyopo katika jamii kutokana na matangazo kwamba Vanilla inalipa na bei ya manunuzi ya Vanilla kwa kilo zinazotajwa kuwa ni kubwa sana. Naomba wananchi tuwe watulivu wakati Serikali Inaendelea kufuatilia jambo hii kwa Kina. Aidha kwa wale ambao tayari wamewekeza waweze kufika kwa RPC wa Mkoa wa Njombe kama ambayo Mheshimiwa RC ameagiza ili kujihakiki majina yao.

Nitoe wito kwa wananchi ambao wanakusudia kuwekeza kusubiri kwanza kuendelea na uwekezaji huu uliopo hadi pale serikali itakapojiridhisha ili kuepusha migogoro au sintofahamu ya aina yoyote inayoweza kujitokeza kwa wananchi.

📍Kazi inaendelea
Picha zinaelezea ziara ya leo nilipoongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwenda kufanya ukaguzi wa eneo maarufu lililowekezwa Vanilla wilayani Njombe.
 
Usikubali kuwekeza popote kama fursa inayotangazwa kampuni haijasajiliwa soko la hisa

Waulize tu mumesajiliwa soko la hisa ili niwekeze hisa zangu?

Wengi wametapeliwa mara sijui wekeza kwenye kuku,vanilla sijui shamba umwaligiliaji rufiji nk usiwekeze kwenye kampuni inayojitangaza tu isiyokuwa soko la hisa .ukisikia wekeza shilingi hizi utavuna mara kumi uliza tu mumesajiliwa soko la hisa? wakisema hapana achana nao
 
Ushauri mzuri sana mkuu
 
Leo umeandika madini kwelikweli
 
Kama kuna kenge mmoja alikuja kunitembelea shambani kwangu nafuga kuku wa mayai akananimbia fuga na sungura ,eti sungura mmoja anauzwa mpaka 60000 na soko lake ni kubwa wakati mimi mwenyewe na utu uzima wangu sijawaai kula sungura ,nikasema inamaana sungura ana bei sawa au zaidi ya mbuzi niakona huu ni utapeli pale tu aliponiambia aniuzie vifaranga vya sungura.
 
Mamalia hawana vifaranga,Kuna shida gani huko shuleni!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…