Kimeumana Vanilla Njombe: Ni utapeli mtupu

Kimeumana Vanilla Njombe: Ni utapeli mtupu

Ujumbe wa DC Njombe kissagwakisakasongwa kuhusu VanillaNjombe

📍Serikali bado inafanyia kazi maswali mengi yaliyopo katika jamii kutokana na matangazo kwamba Vanilla inalipa na bei ya manunuzi ya Vanilla kwa kilo zinazotajwa kuwa ni kubwa sana. Naomba wananchi tuwe watulivu wakati Serikali Inaendelea kufuatilia jambo hii kwa Kina. Aidha kwa wale ambao tayari wamewekeza waweze kufika kwa RPC wa Mkoa wa Njombe kama ambayo Mheshimiwa RC ameagiza ili kujihakiki majina yao.

Nitoe wito kwa wananchi ambao wanakusudia kuwekeza kusubiri kwanza kuendelea na uwekezaji huu uliopo hadi pale serikali itakapojiridhisha ili kuepusha migogoro au sintofahamu ya aina yoyote inayoweza kujitokeza kwa wananchi.

📍Kazi inaendelea
Picha zinaelezea ziara ya leo nilipoongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwenda kufanya ukaguzi wa eneo maarufu lililowekezwa Vanilla wilayani Njombe.

Hao ni Deci wamekuja kivingine, sema watanzania ni wasahaulifu.
 
Haooo jamaa uliowatajaa ni shida tupuu Mkuuu

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Hayo majizi na kitaasisi Chao uchwara huwalaghai watoto wengi wanaoingia chuo,maboom yao huishia kutapeliwa Kwa sababu ya tamaa za kutaka kudouble pesa wapate nyingi maana Hao kenge wanapotoa motivation speaker utajisemea pesa si ndio hii aiseee
Ukishatoa tu pesa jiandae kupigwa na kitu kizito kichwani!
 
HIvi vyombo vya habari vinastahili kuwa na watu wa ethics! Wanatoa matangazo yaliyobuniwa kuwalaghai wananchi yaonekane ni taarifa muhimu ya kitaifa. Ni mengi, ikiwa ni pamoja na yale ya tatu mzuka, Biko,... Kwa mwananchi wa kawaida anahadaika kwamba ni tangazo la kitaifa, kumbe ni utapeli wa aina fulani.

Miaka ya zamani EAC ilikuwa na matamngazo ya dawa ya Aspro, ikisema aspro mbili kwa magonjwa ishirini. WHO ilipiga marufuku tangazo la aina hiyo kujitokeza kwenye vyombo vya habari. Hawa ni washenzi tu na vijineno vya uchumi eti economies of sclale.

Kwa mwenye uelewa kama mimi, nikisikiliza mahojiano ya mkuu wa mkoa na huyo anayejiita muwekezaji, hitimisho ni kwamba muwekezaji ameingiza utapeli, simple. Kivutio ni bei ya milioni 1 kwa kilogram ya vanilla, ambayo amesema ni uongo. What NEXT??

Angalia dakika ya 6:07 ya video hii kama bado umeshupaa shingo.

Dakika ya 12.52 afande anasema kuna "maromanzi". Hivi hicho kitu "maromanzi" ni kitu gani?
 
Kilimo cha ukweli kinacholipa maradufu na kwa haraka ni kilimo cha Bangi ila lazima uisome PGO yote uelewe haki zako za msingi unapokuwa chini ya mikono salama ya serikali kabla ya kushika jembe[emoji205]
Kweli wewe ni cannabis sativa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kilimo cha ukweli kinacholipa maradufu na kwa haraka ni kilimo cha Bangi ila lazima uisome PGO yote uelewe haki zako za msingi unapokuwa chini ya mikono salama ya serikali kabla ya kushika jembe[emoji205]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wewe ni mgeni labda vanilla inalipa Ina pesa ndefu hata kabla ya ujio wa hamasa hii.
Uliza kagera.
Madagascar mashamba ya vanilla yanalindwa na bunduki ndo ujue pesa ipo.
Ilikuwa ni jukumu la serikali kuwaunganisha wakulima na masoko.
Kagera na Madagascar ipi Acha uongo wewe hata Kula hujala unadanganya wenzako
 
Kuna hawa jamaa wanajiita JATU. Kauli mbiu yao ni "Anza na ekari moja"

Mwenye kuwafahamu zaidi atupe msaada.
 
Usikubali kuwekeza popote kama fursa inayotangazwa kampuni haijasajiliwa soko la hisa

Waulize tu mumesajiliwa soko la hisa ili niwekeze hisa zangu?

Wengi wametapeliwa mara sijui wekeza kwenye kuku,vanilla sijui shamba umwaligiliaji rufiji nk usiwekeze kwenye kampuni inayojitangaza tu isiyokuwa soko la hisa .ukisikia wekeza shilingi hizi utavuna mara kumi uliza tu mumesajiliwa soko la hisa? wakisema hapana achana nao
Mkuu umemaliza
 
Naunga hoja
 
Back
Top Bottom