Kimewaka wananchi Tegeta A wamvamia mwenyekiti kisa ubovu wa barabara, wasema wamechoka

Kimewaka wananchi Tegeta A wamvamia mwenyekiti kisa ubovu wa barabara, wasema wamechoka

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Wananchi wa Mtaa wa Tegeta A katika Kata ya Goba wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam, wameandamana mpaka ofisi za Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tegeta A, wakitaka ufafanuzi juu ya sababu zinazopelekewa Barabara ya Tegeta A- Goba Mpakani kubaki kuwa mbovu, licha ya ahadi walizoahiriwa mara kadhaa kuwa Barabara hiyo itajengwa Kwa kiwango Cha lami kupitia mradi wa DMDP.

Katika maandamano hayo yaliyoambatana na vilio vya wakinamama, Wananchi hao wameufikishia uongozi wa Ofisi hiyo malalamiko kadhaa ikiwemo changamoto wanazozipata kupitia ubovu huo wa Barabara, ikiwa ni pamoja na kupanda Kwa nauli, na wajawazito kujifungulia njiani.

Akitoa ufafanuzi wa malalamiko ya Wananchi hao, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tegeta “A”, Proteus Ruwanda amewataka wananchi kuwa wavumilivu huku wakiwasiliana na mamlaka husika kuangalia angalau hata kabla hawajaweka kiwango cha lami, wapitishe greda ili isaidie kwa kipindi hiki cha mvua kupitika.

“Watu wa TARURA walituambia Machi 3, 2025 Barabara zote zenye mradi wa DMDP awamu ya pili zitasaini mkataba, na ilivyopita Tarehe husika nilifuatilia na nikammpigia Meneja wa TARURA akasema wanazifuatulia hizo taarifa, nilifuatilia Tena na Ijumaa akaniambia mkataba wa DMDP upo kwa Mwanasheria Mkuu na haujasainiwa, kwahiyo na sisi bado tunafuatilia kujua utasainiwa lini, na kwasababu waandishi wa habari nao mmekuja, niziombe Mamlaka akiwemo Mkuu wa Wilaya watusaidie, Barabara ni mbovu na athari ni kubwa na kipindi cha mvua kinachokuja gali itakuwa mbaya zaidi,’ amesema Ruwanda.
 
Back
Top Bottom