Kimhemko na kisiasa Makonda yupo sahihi; kitaalamu Mchengerwa Yuko sahihi zaidi!

Kimhemko na kisiasa Makonda yupo sahihi; kitaalamu Mchengerwa Yuko sahihi zaidi!

Dr wa Manesi

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2024
Posts
997
Reaction score
1,220
Usahihi wa Makonda;
Inaweza ikaamsha watendaji kuwahi majukumu yao kwa haraka na kwa wakati.........si mbaya.

Usahihi wa Mchengerwa;

Desturi hii ikiingia katika akili na damu za watu wetu, ambao wengi wao uelewa wao ni mdogo sana na ambao huchagizwa na mihemko ya kisiasa au kikanda na kikabila wakati mwingine, basi hakutakuwa na atakayebaki salama hata huyo Makonda mwenyewe.

-Kuna siku atapigwa kiongozi kisa gari yake imepata ajali.
-Kuna siku polisi zaidi watapigwa na kuuawa kisa wamezuia wananchi wasimuue mwizi waliyemkamata.....
-Kuna atapigwa mtu na kudhalilishwa, kisa hajatoa mchango wa chakula shuleni....
- n.k

Watu waliohemshwa hawana reasoning, wao ni kutafuta sifa tu basi.

Matokeo kwa Sasa;

Makonda atashinda kwa watu sababu taifa limejaawa na wengi wasio na elimu Wala uelewa.Ni mihemko tu.

Atashinda sababu taifa limejaa watu wenye roho mbaya ambao kumharibia yule na yule aliye juu yao ni furaha kuu kwao. Limejaa watu wavivu ambao kujituma na kushirikiana kumaliza kero rahisi tu kwao ni mtihani mkubwa....n.k

Uhusiano wa Makonda na Mchengerwa;

Makonda hatomchangamkia Mchengerwa kamwe, narudia, kaaaaamweeee! Akiwa ni mtu anayejihisi ni mwenye akili kuwazidi wote, kukosolewa kule hatokufurahia kabisa kabisa na, believe me, ameliweka hilo katika moyo wake.

Akiwa ni mtu mpenda kusikilizwa zaidi kuliko yeyote yule, hili limemiwaza.

Akiwa ni mtu wa visasi, hili ataliweka moyoni daima.

Huko mbele akipata madaraka zaidi, Mchengerwa jiandae kutumbuliwa nae.
 
Utawala wa Sheria una misingi yake ndio maana kila kiongozi anaapa kuheshimu katiba na Sheria.
 
Back
Top Bottom