PostGE2025 Kimiti: Kuandamana siku ya Uhuru ni kumvunjia heshima Mwalimu J.K Nyerere

PostGE2025 Kimiti: Kuandamana siku ya Uhuru ni kumvunjia heshima Mwalimu J.K Nyerere

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Wale wazee walikuwa wanahutubiwa alikuwepo
 
CCM ilianza kumvunjia heshima kingali yuko hai,sembuse amekufa?
 
Mzee Paul Peter Kimiti tunakuheshimu sana punguza kutukwaza.
 
Mmeuwa watu elfu 23 plus,unakibuli gani cha kuongea hivyo??,mmezika miili ya wapendwa wetu kama kuku waliokufa na kideli,bado mkawanyima watu kuzika miili ya wapendwa wao,mkapola uchaguzi,bado mnateka,mnabaka,mnalawiti,mnafira na mnauwa,hivi nyinyi ni wanyama au majini??
unajua elfu 23 wewe? acha ujinga waliokufa wengi wahuni na majambazi, nasema wengi sio wote
 
Kuna ubaya gani ukipatikana uhuru wa pili, kwa mnza ndio vizuri, siku za uhuru zitakuwa hazitofautiani😂🤣
 
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere, Paul Kimiti amewataka wanaopanga kuandamana Desemba 9, 2025 kuacha hatua hiyo, akisema wakifanya hivyo watamvunjia heshima mwasisi wa Taifa hili.

Kimiti aliyewahi kuwa waziri na mkuu wa mkoa kwa nyakati tofauti, amesema Desemba 9 ni siku ambayo Tanzania ilipata Uhuru wake, hivyo si vyema kufanya maandamano hayo kwa kuwa tarehe hiyo ina historia kubwa katika Taifa.

Mwanasiasa huyo mkongwe, ametoa kauli hiyo leo Jumapili Desemba 7, 2025 wakati akizungumza na wanahabari nyumbani kwake Ununio kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea nchini.

“Desemba 9 ni siku ya kuomba na kushukuru Mungu ya kwamba tunalinda uhuru, umoja, amani na usalama wa Taifa letu. Tuendelee kumuomba Mungu huko aliko na Mwalimu (Nyerere) atatuombea,” amesema Kimiti.

Wakati Kimiti akitoa rai hiyo, tayari polisi limeshatangaza kupiga marufuku maandamano hayo yanayodaiwa kupangwa kufanyika Desemba 9, ikisema yamekosa nguvu ya kisheria kufanyika ikiwemo wahusika kutotoa taarifa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.
View attachment 3512674
Chanzo: Mwananchi
Katika zile billioni za Rugemalira na kundi lao hakuwemo.
 
Back
Top Bottom