Kimuhemuhe cha Harusi Chaua

Kimuhemuhe cha Harusi Chaua

Hongera kwangu ambaye nilifanya harusi kwa laki 7 na ushee tuu, na life linazidi kuchanja mbuga hapa.

Wapumzike kwa amani, honeymoon wataipata huko huko kwa Muumba wao
Kabisa, huna tofauti na jamaa yangu alifanya arusi ya laki tano, mixer na ndafu ya kuku jogoo kuchi miguu mirefu, kwanini ujitie hasara isiyo ya lazima.
 
Mimi Ni Mkristu mkatoliki.....

Wakati wa kufunga ndoa niliongea na padri tufunge siku ya kazi J3 asubuhi ofisini kwake tukiwa na wadhamini na wazazi mashahidi tu.......

Aliyekuwa Mke akapokea kwa kusitasita....kuwaambia ndugu zake maana wanajiweza wakalipuka kwanini afanye hivyo, Hana ndugu? Hana majirani? Au hachangiagi mtu....mean sio social..... Waafrika sisi.

Baada ya kuona kimdomomdomo hiko nikajipanga na kisalary CHANGU na wazazi wangu wawili Baba na Mama TU..... Mzee anafuga akatoa mbuzi nane.....changanya na kuku mdondo (za kisasa hizi) 15.... Bia tukaongea na jamaa family friend anayza jumla akaleta mzigo wa kutosha ...crate Kama 70 akasema mtalipia mtakazotumia tu....tulirudisha crate 25.....

Mawine kidogo Tena Yale maaltare wine from Moshi Catholic bookshop..vidumu vya Lita tano ..vant,nyagi.....nk nk nk

Then kwa msimamo wangu ambao ulipingwa Hadi na wazazi nikafanyia sherehe nyumbani.....maturubai kodisha mpambaji Kama kawa na mziki mnene....okoa gharama za ukumbi....

Tulitoka church Hadi ndugu wameona aibu wakaleta msafara nikaukataa na mdhamini naye akakataa, namshukuru alikuwa na msimamo mkali kuliko Mimi....hao kwenye kicarina Cha mdhamini na anaendesha mwenyewe mpaka hotel flani ya Lutherani pale juu ya CCP Moshi kwa geti la nyuma huku panaitwa Uhuru, poteza muda Kama masaa mawili.....

Ndoa ilifungwa saa nne aubuhi....sherehe ilianza saa Saba mchana....saa kumi na mbili kwisha.....

Hakuna aliyepewa kadi ya mchango ila wale wa kuona aibu kwasababu tunatoaga waliposikia walitoa wenyewe.......Hawa nawaheshimu maana hawakuombwa Wala kupewa kadi ya mchango.........

Matokeo yake.....
1. Hakuna alalamika as hawakuchanga...
2. Sherehe ilipendeza....
3. Iliweka historian...
4. Nilifanya kitu ndani ya uwezo wangu.....hakukukopwa mahali popote.

Mpaka leo sipati kadi ya mchango wa Harusi hovyo hovyo maana na Mimi sikuwapa watu kadi hovyo hovyo.....

Fanya kitu ndani ya uwezo wako....
 
Kabisa, huna tofauti na jamaa yangu alifanya arusi ya laki tano, mixer na ndafu ya kuku jogoo kuchi miguu mirefu, kwanini ujitie hasara isiyo ya lazima.
Mimi tulijichanga ndugu wote hatukutaka kuwapa watu tabu ya kuchanga, na ndio jambo nilikuwa silitaki maana ni usumbufu sana kwa watu
 
Okeeey, nimeshinda poa kabisa mimi, hivi viswahili bana, sijajua kama umeendeleza kale kasalamu, mana nilishasahau eti, niko nasonga mbele mimi[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Muone kwanza jamani!!
 
Write your reply...Mimi mwenyewe nasubir haka ka bajeti wanakopanga upande wa baba mkwe wangu na michango kadhaa inayohusu harusi maana wameamua kugharamia kila kitu baada ya Mimi kuwa sina kitu wamenipa ka usimamizi mkuu hivo lazima nikimbie na hzo hela kabinti kao kenyewe sikapendi
 
Back
Top Bottom