CCM hawako hivyo unavyofikiria. Hawampi mtu kura kama nafasi zao za ulaji zitakuwa mashakani. Ila kama atawaahidi na kuwahakikishia kuendelea na Uenyeviti na ukatibu wa mikoa wa CCM, Ukatibu mkuu wizarani, ukurugenzi, ukuu wa polisi, ukuu wa magereza, ukuu wa majeshi, ukurugenzi wa halmashauri za miji, uenyekiti wa tume ya uchaguzi na ukurugenzi wake, ukuu wa usalama wa Taifa, Ukuu wa TAKUKURU, Usajili wa vyama vya siasa, Ukuu wa mikoa na wilaya basi siyo tu watampigia kura bali pia watakuwa tayari kumtangaza pindi akichaguliwa na wananchi na hawatamuibia kura. Hao wote niliyowataja ndiyo sababu za kwa nini "CCM huwa inashinda kwa vyovyote au kwa lazima"