Kwetunikwetu
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 1,535
- 412
Mzee wetu Mhe. FREDERICK SUMAYE atueleze nini kinaendelea kati yake na viongozi wakuu wa CHADEMA? Ni juzi tu tarehe 16 Juni majira ya sa 3.15 asubuhi maeneo ya Protea Hoteli iliyopo Oysterbay nilimuona kwa MACHO YANGU mheshimiwa huyu akiwa kwenye gari yake aina ya Landcruiser namba T634 AKN akipokelewa na vigogo wa CHADEMA akiwemo Mhe. MBOWE, DR. SLAA na aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA BOB MAKANI na kuelekea kwenye chumba cha mikutano. Walijifungia kwenye chumba hicho takribani saa mbili na zaidi hadi mishale ya saa 5.20 hivi asubuhi ndipo kigogo huyu alipoondoka eneo hilo. Uswahiba huu umeanza lini??
Nampa HEKO! Napenda kumweleza kuwa kama CHADEMA wamempenda basi atueleze tumpigie debe kwani hadi sasa CHADEMA haijawa wazi nani atagombea kinyangányiro cha kiti cha Urais mwaka huu wa uchaguzi. Pengine bado CHADEMA wanawinda majeruhi wa CCM??
Rai yangu kwa Mheshimiwa SUMAYE ni kwamba, haki kikatiba anayo inayomlinda katika upigaji na upigiwaji wa kura ila mzee, wenzio wa upande wa pili wanayo taarifa hiyo? Au unacheza rafu?
Namtakia kila lililo kheri kwenye mazungumzo yake kuelekea utekelezaji wa demokrasia.
Kuwa wazi, usijifiche una kila haki.
mimi, Chilomo Chiwale
Embu tueleze na wewe ulikuwa unafanya nini hapo? Wewe ulienda kufanya mkutano na nani?