Kimya cha mshana Jr

Kimya cha mshana Jr

Hahaha kumbe mdogo wangu ukipotea kidogo tu wengi wanakumiss. Kumbuka na mimi nilishapost kukuulizia.
 
Naomba kuhoji hasa ukizingatia kuwa ni mmoja wa vigogo waandamiz wa jf. Msaada mkubwa Sana Kwa Maada zake za kufikirisha na kukumbusha.. Sijamwona zaid ya week mbili.. Kapatwa na nini au ndo yuko chaka akirudi na story kubwa kama Ile alivoenda Lindi akakutana na jamaa anayekula popote na kutumia Bila kulipa hela. Uncle mshana Jr. Tumekumiss (tumekukosa). Na sio yeye tu wapo wengi ambao toka haya masakata ya kupelekesha kibabe Babe yaanze hatujawaskia. Siwezi kuwataja wote.. Huu upepo utapita tu na jf itarudi kwenye Zama zake za kuchangamka.. Watu wamekuwa wanyonge Sana ni kama tunasubiria kunyongwa. Mixer stress.. Mixer uwoga mixer kuchanganyikiwa.. Popote ulipo kumbuka lolote linatokea, usifanye makosa.. Tupo Zama za hatari kuwahi kutokea.. Take care... Mwenye mawasiliano na mshana Jr amshutue aje kutupa point chache za namna ya kuishi tanzania ya Sasa.. Maana kukutana na mtu anaongea peke yake barabarani sio ajabu tena Kwa kipindi hiki.
Yupo Dodoma na Lizaboni wanamvizia Bashe na Mibegi yake ya Hela.
 
Back
Top Bottom