Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Watanzania tunaendelea kushangazwa sana na kimya kizito kinachoendelea Cha Rais Samia, kuhusu kifo Cha kiongozi wa CHADEMA, Ali Kibao kilichotokea tarehe 7 mwezi uliopita.
Nakumbuka Rais Samia ali-react mapema sana baada ya kusikia kifo hicho kilichotokea tarehe 7 mwezi uliopita na mwili wake kutupwa huko Kwenye kichaka, maeneo ya Ununio.
Nipende kunukuu post yake aliyoi-post kwenye ukurasa wake wa X, zamani Twitter kama ifuatavyo:-
"Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya kiongozi wa CHADEMA, Ali Kibao, natoa pole Kwa viongozi wa chama hicho, familia, ya Mzee Kibao, ndugu na jamaa zake.
Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii HARAKA.
Nchi yetu ni ya kidemokrasia na Kila raia ana HAKI YA KUISHI.
Serikali ninayoiongoza HAIVUMILII vitendo vya kikatili vya aina hii"
Mwisho wa kunukuu
Hivi sasa inakaribia mwezi mmoja tokea tukio hilo baya kabisa, litokee naona bado kimya kizito kinaendelea kutawala kuhusiana na kifo hicho, ambacho kimetuharibia sana sifa yetu kimataifa kuwa hii nchi ni ya amani
Watanzania tungetegemea baada ya hili tukio baya kabisa kutokea, Moja Kati ya haya mambo mawili yatokee.
Aidha Waziri wa Mambo ya ndani, Yusuph Masauni, DGIS, Suleiman Mombo na IGP, Camilius Wambura wajiuzulu mara moja au mamlaka iliyowateua, ambayo ni Rais iwatengue.
Kwa bahati mbaya sana, hakuna lolote lililotokea Kati ya hayo mambo mawili!
Chama Cha CHADEMA, kiliandaa maandamano yake ya amani tarehe 23 mwezi uliopita, Ili kuomboleza kifo Cha kiongozi wao Ali Kibao aliyetekwa na baadaye kuuawa kinyama na kulitaka Jeshi la Polisi, lieleze wako wapi viongozi wao waliotekwa, akina Deus Soka na wenzake.
Hata hivyo maandamano hayo ya amani, ambayo yanaruhusiwa Kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu, hayakufanyika kutokana na Jeshi letu la Polisi kuyapiga marufuku na kuimarisha ulinzi wa hali ya juu, jijini Dar.
Aidha Chama Cha CHADEMA kimemtaka Rais Samia aunde Tume huru ya kijaji, pendekezo ambalo pia inaelekea limekataliwa na Rais Samia.
Kwa kuwa kama akivyoeleza Rais Samia mwenyewe kuwa nchi yetu ni ya kidemokrasia na Kila raia ana HAKI YA KUISHI, sasa sielewi ni kwanini anagomea kuundwa Kwa Tume huru ya kijaji , kuchunguza kifo hicho Cha Ali Kibao??
Sasa ningependa kumuuliza Rais Samia, je huo uchunguzi ulioutaka ufanywe haraka iwezekanavyo na ripoti ya uchunguzi huo ikufikie wewe, bado haijakufikia Hadi sasa inakaribia mwezi mmoja tokea tukio Hilo limetokea??
Swali la Pili, hivi inakuwaje katika tukio baya hili kama wewe mwenyewe ulivyonukuliwa ukisema katika post yako katika ukurasa wako wa Twitter, leo inakaribia mwezi mmoja, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na serikali yako??
Kwa kweli katika hatua tuliyofikia Taifa hili, inabidi wananchi tuendelee kuliombea Ili lirejee kuwa ni Taifa la Amani kama lilivyokuwa hapo awali.
Mungu ibariki Tanzania