Evelyn Salt
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 70,916
- 141,437
Amani iwe kwenu,
Napenda kushare hili, tabia ya sisi kina dada kushindwa kutambua na kuthamini nafasi za mawifi zetu kwa makusudi, kwa kujitoa ufahamu au kutokujua kwa bahati mbaya, hadi inafikia mahali tunakua na maamuzi yasio ya lazima kwa kaka zetu.
Wapendwa hakuna mtu asietambua umuhimu wa ndugu kwani wao ndio wanajua wapi wametoka, mangapi wamepitia pamoja hadi kufika mahali walipo, lakini sidhani kama ni sababu ya kushindwa kutambua na kuthamini kuwa ndugu (kaka) ameishaongeza jukumu lingine (mme) kiasi kwamba kuendelea kujiona kwamba dada una uhuru wa maamuzi kwake.
Undugu upo palepale tena upo sana lakini ni vema maamuzi ya kaka kwa mambo ya familia aachiwe mkewe (wifi), labda tu kama dada umeombwa ushauri,binafsi naona kumfanyia kaka maamuzi wakati tayari ana mkewe ni kutafutana tu migogoro na wifi na inawezekana hata kuwa moja ya sababu za mawifi kutopendana mfano dada kumpangia kaka ake matumizi na mgawanyo wa pesa kiasi hiki kaka nunua kioo, kiasi kile nunua mswaki na kiwi kingine peleka bank wtf!
Nafasi ya mke ni nini sasa? Tutajatukanwa mambo ya nguoni jamani tuone tumeonewa, hivi hata wifi akija gundua dada mtu ndio mpangaji wa matumizi ya nyumbani kwake atajisikiaje?Na kaka nae anawezaje kuruhusu huu ulofa katika familia yake?
Inawezekanaje dada kwenda kwa kaka na kujimwaga mwaga hadi chumbani kwake ilhali sio geto ni chumba chake na mkewe?inawezekana kukaa na kaka na unamlisha chakula ilhali mkewe yupo? Uzungu au rusha roho?
au kutembea njiani na kaka mshikane mikono afu mke pembeni kajibebea zake kipochi, ni upendo wa ndugu sawa, ila huwa hauna mipaka? Tunapenda ndugu zetu tena upendo wetu haupimiki lakini ni vema upendo uwe na mipaka especially ndugu zetu wakishajiongezea jukumu lingine la mke/mme ni hayo tu ni mawazo yangu tu we unawazaje?