Kina dada tupunguze maamuzi yasio ya muhimu kwa kaka zetu waingiapo kwenye ndoa zao

nashukuru kupata dada mwelewa, ambaye anapika na kupakua na mtu wangu hadi mwenyewe huwa anamsifia
 
Kama nakuona tatty ndo wifio, yale mahaba ulionayo kwa kaka ako mbona wifi atajuta kukufahamu

Hahahaaa....unajua kuna watu wamekariri na pindi wanapoingia ndoani wanatoka wamejiandaa kabisa kupambana...muombe Mungu upate familia nzuri sio unavaa gloves kabisa
 
Hujui mawifi wasumbufu mara nyingi ni wale tegemezi na walioachika kwenye ndoa au Hawajawahi kuolewa. Hahahahahaha!!!

Watu asubuh 12 unawakuta mlangoni. Sina ham nao hawa watu aisee!!
Kuna bidada mmoja ana hii type ya mawifi, akinisimuliaga anakua na uchungu hadi ataka kulia ha ha ha
huyo wifi ni mkubwa tu wa kutosha, ana miaka 30 ila kwa kua ni last born basi anajiona kama yupo la tatu B hadi hela ya kyupi anategemea kwa kaka mazafanta kabisa!!!
kuna kipindi akaja kuishi kwa bro wake (hapo wana chumba tu kimoja na sitting room) ila ana dada ambae anaishi mwenyewe, sasa sijui kwanini hakwenda kuishi kwa dada ake akaja kubanana kwa kaka mwenye chumba kimoja
humo ndani utadhani kuna wake wawili
 
Ha ha ha bana eeeh ndo maana refa anaingiaga uwanjani na kadi nyekundu, kwa anatakaga watu wachezeane rafu? Teh
 
unaanzaje kuingilia ndoa yangu kama wifi?? sahau kabisa maana ukijaribu siku ya 1 tu sikufumbii macho

Wapo wadada na wakaka wanaoingilia NDOA na Kama kwako hawajafika ni jambo la kumshukuru Mungu. Mimi nimeona mama zangu wanavo waonea mawifi zao, japo wao ni wakali balaaa kwenye NDOA zao.
 
Yaani hizi shida za mawifi sijui mwisho wake, wajuvi wa saikolojia wanaweza wakatujuza zaidi, ila ni jukumu la mwanaume kuchukua nafasi ya kutenga mambo ya familia yao na ya nyumbani kwake, kila kimoja kiwe na nafasi yake na sio kuingiliana kwa kiasi hicho.
Ndio hadi mwanaume awe na hiyo akili ya kutenganisha familia na ndoa
la sivo utaonekana mke una roho mbaya, una gubu, hupendi ndugu wa mme na kila kesi itakuandama
 
Hujui mawifi wasumbufu mara nyingi ni wale tegemezi na walioachika kwenye ndoa au Hawajawahi kuolewa. Hahahahahaha!!!

Watu asubuh 12 unawakuta mlangoni. Sina ham nao hawa watu aisee!!

Neno kabisa, namjua mmoja bwana mama ni msumbufu kwa mawifi zake kinomaaaa, sasa kahamishia familia yake kwa kaka yake na toto lake kubwa limemaliza chuo wote wanakaa hapo kwa kaka. Basi wifi wa japo home hafurukuti, wifi mwenyewe mzeee, wakati mke ni binti mdogo tu.
 
Kuna bidada mmoja ana hii type ya mawifi, akinisimuliaga anakua na uchungu hadi ataka kulia ha ha ha
huyo wifi ni mkubwa tu wa kutosha, ana miaka 30 ila kwa kua ni last born basi anajiona kama yupo la tatu B hadi hela ya kyupi anategemea kwa kaka mazafanta kabisa!!!
kuna kipindi akaja kuishi kwa bro wake (hapo wana chumba tu kimoja na sitting room) ila ana dada ambae anaishi mwenyewe, sasa sijui kwanini hakwenda kuishi kwa dada ake akaja kubanana kwa kaka mwenye chumba kimoja
humo ndani utadhani kuna wake wawili

Wallah siwez kubali ataondoka kama alivyokuja 30yrs bado unategemea vya kaka hadi ch*pi hapana kwa kweli labda awe mlemavu
 
Ha ha ha bana eeeh ndo maana refa anaingiaga uwanjani na kadi nyekundu, kwa anatakaga watu wachezeane rafu? Teh

Hahaa ndio maana yule mwanamke alikuwa ananitolea mijicho balaa....ila mi sinaga taimu na mtu
 
Ndio hadi mwanaume awe na hiyo akili ya kutenganisha familia na ndoa
la sivo utaonekana mke una roho mbaya, una gubu, hupendi ndugu wa mme na kila kesi itakuandama

Alafu ukute huyo mwanaume anawatetea ndugu zake sasa!! Yaani kuna wanaume wanakera jamani utadhani walipewa tu hiyo jinsia ya kiume!!
 
Kuna bidada mmoja ana hii type ya mawifi, akinisimuliaga anakua na uchungu hadi ataka kulia ha ha ha
huyo wifi ni mkubwa tu wa kutosha, ana miaka 30 ila kwa kua ni last born basi anajiona kama yupo la tatu B hadi hela ya kyupi anategemea kwa kaka mazafanta kabisa!!!
kuna kipindi akaja kuishi kwa bro wake (hapo wana chumba tu kimoja na sitting room) ila ana dada ambae anaishi mwenyewe, sasa sijui kwanini hakwenda kuishi kwa dada ake akaja kubanana kwa kaka mwenye chumba kimoja
humo ndani utadhani kuna wake wawili

Mi hua siku nikivurugwa nilikuwa nawaambia nimeolewa na 1 sio 11 kwa hiyo kila mtu atulie kwenye mji wake alee familia. walikua wanajikusanya watu 6 wanahamia kwangu jamani jamani wengine wanawatoto wadogo, yaani nilikua kama nina kidispensary sasa siku masanja akatioa vijembe kwenye original comedy wakati wote tunaangalia, dah!!!!! nikaona watu wanaaga mmoja mmoja.
 
Neno kabisa, namjua mmoja bwana mama ni msumbufu kwa mawifi zake kinomaaaa, sasa kahamishia familia yake kwa kaka yake na toto lake kubwa limemaliza chuo wote wanakaa hapo kwa kaka. Basi wifi wa japo home hafurukuti, wifi mwenyewe mzeee, wakati mke ni binti mdogo tu.

Wana hila sana, mimi hadi sipendi kuitwa wifi na wake wa kaka zangu, maana nalionea kichefuchefu hili jina.

Hehehehe hata mimi natamani hivohivo

Watapita watasoma tu.
 
Wallah siwez kubali ataondoka kama alivyokuja 30yrs bado unategemea vya kaka hadi ch*pi hapana kwa kweli labda awe mlemavu
Mtu mzima na akili zake hana ulemavu wa mwili, labda kama kichwani kwake kuna nati zimelegea
make alivokujaga tu kabla sijatambulishwa nkahisi tu kutokana na story atakua ni yeye
anaamka saa nne na skin tight yake anaswaki anakaa miguu juu na remote mkononi
ni kuagiza tu wifi niwekee chai kiasi akila vyombo hajigusi kutoa, analiendeleza hadi mchana analetewa msosi hapo hapo
ila kaka anachangia hiyo
 
Duh! Wanawake mna kazi sana.

Wakati sisi tunapiga Monde na mashemeji zetu , nyie mmekaa na mawifi zenu kimitego mitego.
You better learn to love each other, otherwise hamtaweza kuwa na maisha yenye utulivu.
 
Back
Top Bottom