Kina dada tupunguze maamuzi yasio ya muhimu kwa kaka zetu waingiapo kwenye ndoa zao

ila sasa awaza lile tunda ntapata wapi? dada namtaka na tunda nataka.....mtihani huu

Tunda utajua hatma yake ukishafika kwa dada ha ha ha au muombe ushauri dada ako
Au waweza chukua sabuni ukafanye mambo ya nape
 
Kuna story moja mke alipoona Wifi kazidi alimualika chumbani huku akijua kaka mtu(mume) dushelele iko 90 degree akamwambia njoo utoe huduma kwa kaka yako.

Hahahaaaa! Watu wamepinda!!
 
Kwa kweli inakera sana...usiombe yakukute,mi nimepata mpaka vidonda vya tumbo kwasababu ya ndugu Wa mume wangu
 
Ni wajibu wangu kuwasaidia ndg zangu pale ninapokuwa na uwezo wa kufanya hivyo lakini nitakapooa haiingii akilini Mdogo wangu wa kike kuingia chumbani kwangu...hata sasahv si ruhusa kufanya hivyo labda kama naumwa na nimezidiwa.
 
mke/wifi wakiwa marafiki kuna kitu kinafanyika out of you kaka
na kutokuwa marafiki ndo kuliko zoeleka
kaka yakupashwa kujitambua kuwa sasa hivi nimeoa na napashwa kuwa na mipaka kwa ndugu na jamaa kama mwanzo kuna majukumu alikuwa anafanya dada basi amepatikana mfanyaji na kama kulikuwa na mazoea tunafanya ambayo yanaweza kumkwaza mwenzio basi yaishie hapo
 
Amani iwe kwenu,

Napenda kushare hili, tabia ya sisi kina dada kushindwa kutambua na kuthamini nafasi za mawifi zetu kwa makusudi, kwa kujitoa ufahamu au kutokujua kwa bahati mbaya, hadi inafikia mahali tunakua na maamuzi yasio ya lazima kwa kaka zetu.

Wapendwa hakuna mtu asietambua umuhimu wa ndugu kwani wao ndio wanajua wapi wametoka, mangapi wamepitia pamoja hadi kufika mahali walipo, lakini sidhani kama ni sababu ya kushindwa kutambua na kuthamini kuwa ndugu (kaka) ameishaongeza jukumu lingine (mme) kiasi kwamba kuendelea kujiona kwamba dada una uhuru wa maamuzi kwake.

Undugu upo palepale tena upo sana lakini ni vema maamuzi ya kaka kwa mambo ya familia aachiwe mkewe (wifi), labda tu kama dada umeombwa ushauri,binafsi naona kumfanyia kaka maamuzi wakati tayari ana mkewe ni kutafutana tu migogoro na wifi na inawezekana hata kuwa moja ya sababu za mawifi kutopendana mfano dada kumpangia kaka ake matumizi na mgawanyo wa pesa kiasi hiki kaka nunua kioo, kiasi kile nunua mswaki na kiwi kingine peleka bank wtf!

Nafasi ya mke ni nini sasa? Tutajatukanwa mambo ya nguoni jamani tuone tumeonewa, hivi hata wifi akija gundua dada mtu ndio mpangaji wa matumizi ya nyumbani kwake atajisikiaje?Na kaka nae anawezaje kuruhusu huu ulofa katika familia yake?

Inawezekanaje dada kwenda kwa kaka na kujimwaga mwaga hadi chumbani kwake ilhali sio geto ni chumba chake na mkewe?inawezekana kukaa na kaka na unamlisha chakula ilhali mkewe yupo? Uzungu au rusha roho?

au kutembea njiani na kaka mshikane mikono afu mke pembeni kajibebea zake kipochi, ni upendo wa ndugu sawa, ila huwa hauna mipaka? Tunapenda ndugu zetu tena upendo wetu haupimiki lakini ni vema upendo uwe na mipaka especially ndugu zetu wakishajiongezea jukumu lingine la mke/mme ni hayo tu ni mawazo yangu tu we unawazaje?
 
Ni wajibu wangu kuwasaidia ndg zangu pale ninapokuwa na uwezo wa kufanya hivyo lakini nitakapooa haiingii akilini Mdogo wangu wa kike kuingia chumbani kwangu...hata sasahv si ruhusa kufanya hivyo labda kama naumwa na nimezidiwa.
 
Ila me nafikiri mwanaume (kaka) ndo anatakiwa asimame kiume (awe na msimamo), otherwise ataendeshwa na madada zake hadi ndoa imshinde. Asipowaruhusu dada zake kumtawala, basi hakuna atakayemtawala. Na huyo dada wa kumpangia kaka ake matumizi yeye hana familia ajipangie matumizi yake khaaa!! Mwanaume ndo kichwa cha familia yake na sio dada zake. Kichwa kikitetereka Kila kitu kitaharibika
 
Amani iwe kwenu,

Napenda kushare hili, tabia ya sisi kina dada kushindwa kutambua na kuthamini nafasi za mawifi zetu kwa makusudi, kwa kujitoa ufahamu au kutokujua kwa bahati mbaya, hadi inafikia mahali tunakua na maamuzi yasio ya lazima kwa kaka zetu.

Wapendwa hakuna mtu asietambua umuhimu wa ndugu kwani wao ndio wanajua wapi wametoka, mangapi wamepitia pamoja hadi kufika mahali walipo, lakini sidhani kama ni sababu ya kushindwa kutambua na kuthamini kuwa ndugu (kaka) ameishaongeza jukumu lingine (mme) kiasi kwamba kuendelea kujiona kwamba dada una uhuru wa maamuzi kwake.

Undugu upo palepale tena upo sana lakini ni vema maamuzi ya kaka kwa mambo ya familia aachiwe mkewe (wifi), labda tu kama dada umeombwa ushauri,binafsi naona kumfanyia kaka maamuzi wakati tayari ana mkewe ni kutafutana tu migogoro na wifi na inawezekana hata kuwa moja ya sababu za mawifi kutopendana mfano dada kumpangia kaka ake matumizi na mgawanyo wa pesa kiasi hiki kaka nunua kioo, kiasi kile nunua mswaki na kiwi kingine peleka bank wtf!

Nafasi ya mke ni nini sasa? Tutajatukanwa mambo ya nguoni jamani tuone tumeonewa, hivi hata wifi akija gundua dada mtu ndio mpangaji wa matumizi ya nyumbani kwake atajisikiaje?Na kaka nae anawezaje kuruhusu huu ulofa katika familia yake?

Inawezekanaje dada kwenda kwa kaka na kujimwaga mwaga hadi chumbani kwake ilhali sio geto ni chumba chake na mkewe?inawezekana kukaa na kaka na unamlisha chakula ilhali mkewe yupo? Uzungu au rusha roho?

au kutembea njiani na kaka mshikane mikono afu mke pembeni kajibebea zake kipochi, ni upendo wa ndugu sawa, ila huwa hauna mipaka? Tunapenda ndugu zetu tena upendo wetu haupimiki lakini ni vema upendo uwe na mipaka especially ndugu zetu wakishajiongezea jukumu lingine la mke/mme ni hayo tu ni mawazo yangu tu we unawazaje?
Umeongea kweli tupu.
 
Back
Top Bottom