Kina dada tupunguze maamuzi yasio ya muhimu kwa kaka zetu waingiapo kwenye ndoa zao

Kina dada tupunguze maamuzi yasio ya muhimu kwa kaka zetu waingiapo kwenye ndoa zao

mmh... huo wivu mawifi mpunguze jamani.
Hamjiamini?

Ila mjiangalie, wengi wenu vimeo hadi waume zenu hawawaamini. Hivi mimi mume wangu anaanzaje kushirikisha ndugu zake masuala ya nyumba yetu? ANANIAMINI hata aache pesa hapo asafiri mwaka mzima anajua mkewe TREKTA.
Akikuona KILAZA lazima atatafuta wa kumsaidia mawazo. Vinginevyo huyo mume nae KIMEO.
 
Mweeh... Nashkuru sina wifi,maana the way nilivyo ningepata tabu kama ningekutana na mawifi waruwaru
 
kuna wifi mpaka mama wakwe wengine nao wasumbufu sana. kutwa maneno tu.

na sisi wanaume tuwe na misimamo.
 
Ila me nafikiri mwanaume (kaka) ndo anatakiwa asimame kiume (awe na msimamo), otherwise ataendeshwa na madada zake hadi ndoa imshinde. Asipowaruhusu dada zake kumtawala, basi hakuna atakayemtawala. Na huyo dada wa kumpangia kaka ake matumizi yeye hana familia ajipangie matumizi yake khaaa!! Mwanaume ndo kichwa cha familia yake na sio dada zake. Kichwa kikitetereka Kila kitu kitaharibika

sasa dada alikuwa ananidunda tangu utotoni, hata miezi kadhaa nyuma kabla ya kufunga ndoa alinidunda....leo anipangie nikatae kweli?? hunitakii mema
 
sasa dada alikuwa ananidunda tangu utotoni, hata miezi kadhaa nyuma kabla ya kufunga ndoa alinidunda....leo anipangie nikatae kweli?? hunitakii mema
Mmh hongera, upigwe vizuri tu
 
sasa dada alikuwa ananidunda tangu utotoni, hata miezi kadhaa nyuma kabla ya kufunga ndoa alinidunda....leo anipangie nikatae kweli?? hunitakii mema
Ungeenda kuishi na dada ako ili usimpe shida mkeo ingependeza zaid
 
Hahaa daaah umenikumbusha....mimi na kaka yangu ninayemfuata tangu tupo wadogo tunapendana kishenz...yan ni marafiki haswaaa...tukikaa pamoja full kutaniana, kupigana,kukimbizana yan full raha. Sasa juzi tu hapa hata kaja kututambulisha mkewe mtarajiwa. Bas my elder sista kaniambia nianze ku-maintain distance maana keshakuwa na wake sasa...yaan ni furaha iliyochanganyika na machungu

Kimya, unitafute ....
 
Back
Top Bottom