Kina mama si kwa kuwachimba huku wakwe zenu wakike

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,559
Reaction score
19,101
Mama yangu ni mtu mzima na ameshaozesha watoto wake kadhaa wakike kwa wakiume ikiwa ni pamoja na watoto wake wa kuwazaa, watoto wengine wa ndugu zake na wengine tu aliyowalea

Siku zote dada zetu wakipata wachumba na kuwaleta kwa utambulisho nyumbani mama hana shinda hua anakua ni mwenye furaha na tabasamu muda wote. Pia anakua ni mcheshi sana kwa wakwe zake hao wa kiume watarajiwa

Kasheshe huja pale mwanae wa kiume anapotaka kuoa au kumtambulisha mchumba. Mama anakua sio mwepesi kukubal,i kwa maana atataka habari za kutosha za huyo mwanamke. Tena itamshughulisha kwa kuchukua hatua za kuwauliza watu wengine na huku akitaka wamfanyie uchungunguzi mkwe mtarajiwa

Kuna kaka yetu alipata mchumba Mwanza, alipokuja kumtambulisha home bi mkubwa alimuuliza maswali mengi sana na mwisho wa siku alifunga safari kwenda huko Mwanza kwa dada yake binamu, safari ambayo baadae tulikuja kujua ilikua ni ya kutaka kutafuta habari zaidi za huyo mtoto wa kike!

Bahati nzuri kwa upande wake alifanikiwa kupata taarifa alizokua anazihitaji kuhusu huyo shemeji yetu na kwa mshangao wa wengi alimkataa huyo binti kuolewa na brother! Pamoja na kaka kulalamika na kupinga mwisho wa siku amri ya Bi Mkubwa ilitekelezwa na sasa hivi kaka ana ndoa na mwanamke mwingine wakiishi kwa amani na furaha

Nilikua nadhani ni mama yetu pekee ndio yupo hivi lakini nilipata nafasi ya kuongea na watu kadhaa kuhusu hili na angalau watu watatu walinithibitishia kua wamewahi kushuhudia kina mama kadhaa wakiwa na tabia hiyo

Najiuliza katika dunia ya sasa jambo hili linanafasi kweli? Na nini hasa sababu ya mama zetu kua very protective kwa watoto wao wa kiume linapokuja suala la kuchagua mwenza wa maisha? Kwanini kina mama hao wa zamani wanawawekea vigezo vingi sana watoto wao wa kiume kuhusu aina ya wachumba wanaowapata wakati kwa watoto wao wa kike hawaweki vigezo vyovyote vya maana kuhusiana na hilo, kwani miminadhani ilipaswa kua kinyume chake
 
Iko hivyo kote aisee akina mama huwa hawajali sana binti anaolewa wapi, ila wanakuwa makini sana kujuchunguza kijana anakooa nadhani ni kwa sababu kijana anapooa analeta mtu mgeni kwenye familia kwa hiyo ni halali mtu kutaka kumjua memba huyu mpya. Wanawake wengine ni akina Yona akiingia tu chomboni bahari inachafuka.
 
Mi naona mama yenu ana malengo mazuri na watoto wake wa kiume hataki usumbufu huko baadae kwa upande wa watoto wake wa kike hapo napo hana wasiwasi nao maana kawalelea na anawajua zaidi
Sometimes tunamuona kama dictator flani hivi hasa ukizingatia alikua mkali sana kwa watoto wake enzi zake. Kwa hiyo anataka kuendelea hivyohivyo wakati watu tushakua wakubwa sasa
 
Inamaana mwanamke muolewaji anaweza leta madhara makubwa kwenye familia anayo olewa kuliko mwanaume anaingia kuoa kwenye familia husika?
 
Nimependa sana kumbe mnajijua
 
Naihusianisha hiyo na Electra complex na Oedipus complex. Mtoto wa kike huwa anampenda baba sana na kumuona mama yake ni rival wa affection yake kwa baba na kinyume chake kwa mtoto wa kiume.

Deep down hawa watu hua na bond inayojengeka kipindi hicho. Kesi nyingi za mama au baba kutembea na mwanae mzizi hua hapo kwenye hizo phenomena mbili.

Nachukulia hata Mama yako/ zetu wanaact hivyo kutokana na hiyo Oedipus Complex.
 
Inamaana mwanamke muolewaji anaweza leta madhara makubwa kwenye familia anayo olewa kuliko mwanaume anaingia kuoa kwenye familia husika?
Of courage, mwanamke akiolewa anakuwa sehemu ya familia kabisa kabisa tofauti na mkwe wa kiume ye anakuwa mwanafamilia ndio lakini sio kiviile ila mtoto wenu ndio mnakuwa mmempeleka kwenye familia nyingine, inategemea na jamii lakini kwa upande wetu iko hivyo
 
Kwa hiyo hapa mama anataka mwanae apate kitu kizuri au ni vipi? Hapo kuna element ya wivu labda kutokana na maoni yako? Au sijakupata vizuri mkuu?
 
Mimi mke wangu nimeshamuachia jukumu hilo mama ... Sipotezi muda
Hiyo wanaita ku outsource jukumu la kutafuta mkeπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Kwa uzoefu wangu kwa mama yetu mara nyingi chaguzi zao zinakua ni chaguzi bora maana wanakua na vigezo vyao vile vya kizamani kuhusu mke na majukumu yake
 
Kwa hiyo hapa mama anataka mwanae apate kitu kizuri au ni vipi? Hapo kuna element ya wivu labda kutokana na maoni yako? Au sijakupata vizuri mkuu?
Hapa sasa itategemea Oedipus Complex ilikua handled vipi. Kama wakati mtoto yuko kwenye hiyo steji na wazazi wakagive in kwenye hii condition basi mama hujikuta kua overprotective, hivyo elements za Wivu zitakuepo na elements za jamaa kua mama's boy zitakuepo.
 
Wanawake wanajuana,yaan mama anamjua huyu mwanamke mzugaj,mdangaji,mkwel ama si mkwel....

Na hata sku1 usimbishie mama yako,sabab utakuja juta,akikwambia mwanangu huyu mwanamke hafai ujue hafai kwel.
Kama kuna ukweli flani hivi nauona ndani ya hoja yako mkuu
 
Oooh, sawa mkuu nitajielimisha zaidi huhusu hizo concepts za Oedipus Complex na Electra Complex niweze kulinganisha na mazingira halisi
 
Hiyo wanaita ku outsource jukumu la kutafuta mkeπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Kwa uzoefu wangu kwa mama yetu mara nyingi chaguzi zao zinakua ni chaguzi bora maana wanakua na vigezo vyao vile vya kizamani kuhusu mke na majukumu yake
Nilishawahi date demu mama aliongea nae kwenye simu tu one day video call.. Akamwambia sister mdogo wako hajapata bado mchumba... Mwezi tu baada ya huyo kauli tukaachana.. Demu ni tapeli tu
 
Oooh, haya mambo yanashangaza kwakweli. Wanawake unaweza kudhani ni dhaifu lakini kumbe anaweza akaolewa sehemu akaingia kwenye familia na ukoo wa watu akaja aka influence mambo na kuleta mabadiliko makubwa sana yawe hasi au chanya, si ndio una maanisha hivyo Khantwe ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…