Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,559
- 19,101
Mama yangu ni mtu mzima na ameshaozesha watoto wake kadhaa wakike kwa wakiume ikiwa ni pamoja na watoto wake wa kuwazaa, watoto wengine wa ndugu zake na wengine tu aliyowalea
Siku zote dada zetu wakipata wachumba na kuwaleta kwa utambulisho nyumbani mama hana shinda hua anakua ni mwenye furaha na tabasamu muda wote. Pia anakua ni mcheshi sana kwa wakwe zake hao wa kiume watarajiwa
Kasheshe huja pale mwanae wa kiume anapotaka kuoa au kumtambulisha mchumba. Mama anakua sio mwepesi kukubal,i kwa maana atataka habari za kutosha za huyo mwanamke. Tena itamshughulisha kwa kuchukua hatua za kuwauliza watu wengine na huku akitaka wamfanyie uchungunguzi mkwe mtarajiwa
Kuna kaka yetu alipata mchumba Mwanza, alipokuja kumtambulisha home bi mkubwa alimuuliza maswali mengi sana na mwisho wa siku alifunga safari kwenda huko Mwanza kwa dada yake binamu, safari ambayo baadae tulikuja kujua ilikua ni ya kutaka kutafuta habari zaidi za huyo mtoto wa kike!
Bahati nzuri kwa upande wake alifanikiwa kupata taarifa alizokua anazihitaji kuhusu huyo shemeji yetu na kwa mshangao wa wengi alimkataa huyo binti kuolewa na brother! Pamoja na kaka kulalamika na kupinga mwisho wa siku amri ya Bi Mkubwa ilitekelezwa na sasa hivi kaka ana ndoa na mwanamke mwingine wakiishi kwa amani na furaha
Nilikua nadhani ni mama yetu pekee ndio yupo hivi lakini nilipata nafasi ya kuongea na watu kadhaa kuhusu hili na angalau watu watatu walinithibitishia kua wamewahi kushuhudia kina mama kadhaa wakiwa na tabia hiyo
Najiuliza katika dunia ya sasa jambo hili linanafasi kweli? Na nini hasa sababu ya mama zetu kua very protective kwa watoto wao wa kiume linapokuja suala la kuchagua mwenza wa maisha? Kwanini kina mama hao wa zamani wanawawekea vigezo vingi sana watoto wao wa kiume kuhusu aina ya wachumba wanaowapata wakati kwa watoto wao wa kike hawaweki vigezo vyovyote vya maana kuhusiana na hilo, kwani miminadhani ilipaswa kua kinyume chake