Kina Mangi njooni tubadilishane uzoefu. Tushirikiane.

Kina Mangi njooni tubadilishane uzoefu. Tushirikiane.

yello masai

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2016
Posts
3,662
Reaction score
3,715
Habari wadau,
Wale wenye maduka ya bidhaa za rejareja (mangi) tukutane hapa tubadilishane mawazo kidogo, tujadili ili kila mmoja aiweke biashara yake kwenyw kipimo kwa kulinganisha na wengine ili tuweze kuboresha zaidi.

Binafsi sina duka ila nna kijiduka au kibanda nilichokianza baada ya kupoteza kazi yangu niliyokuwa nayo mwanzo,

Wakuu mi nitagusia mambo yafuatayo;

1. Mauzo.
Hapa tujue mauzo ya kawaida kwa siku.
Mimi binafsi siku hazilingani, siku za j3 na j4 mauzo hushuka sana na kufikia angalau 120K kwa siku. Siku zingine hupanda kidogo mpaka kwenye 170, 150,... Siku za jmos na jpili mauzo hufika laki mbili au zaidi kidogo kwa siku.

2. Ushindani.
Hapa wakuu tushee picha halisi ya mazingira tunayofanyia biashara, na unakabiriana vipi na changamoto ya ushindani.
Binafsi mi nilipo nilikuta maduka mawili, mimi nikawa wa tatu. Mmoja wetu ana duka na genge, hivyo wateja wengi hupenda kwenda pale kwa sababu wanapata huduma zote kwa pamoja. Mi niliona nifanye tofaut, nikamix bidhaa za kawaida na nyingne kama baadhi ya vifaa vya umeme (taa, holder,..) Makufuli, etc.. maana niliona huduma hizi hakuna hapa mtaani, imenisaidia kufanya nizoeleke maana wateja wengine huja kufata vitu hivyo baada ya kuvikosa kwa hawa wenyeji.

3. Imani.
Wengi uhuhusisha hizi biashara na imani za kishirikina, na huenda sana kwa waganga kutafuta kitu kinachoitwa mvuto au king'amuzi.
Binafsi naamini hayo mambo yapo na watu wanachangamsha sana biashara zao kupitia mambo haya. Lakini mimi sijawahi kujihusisha na sina mpango sababu mambo haya huchukua hela nyingi na ukishayaanza ni ngumu kuacha. Vile vile mwisho wake mara nyingi sio mzuri.
Je nyie wadau mnalichukuliaje suala hili? Je wewe huwa unaenda?

4. Faida. Je hii biashara ina faida? Na ni kiasi gani? Unaijuaje au unaiona kwa namna gani hiyo faida?

Binafsi huwa sicomplicate, kila siku nachukua elf 20 naweka akiba. Haijalishi nimeuza kiasi gani.
Chakula cha kupika kinatoka dukani pamoja na mahitaji mengine, (hiyo yote ni faida). Lakini ninatoa kwa umakini sana. Na biashara yangu haijawahi kurudi nyuma, zaidi naongeza bidhaa mpya na kupanua kidogo kidogo.

Nawakaribisha wote wenye biashara ya namna hii tujadili, tubadilishane uzoefu, tufundishane, tufunguane, tunaeza pia kugusia na mengine zaidi kama namna ya kununua bidhaa, sehemu za kununua na mengine mengi.

Karibuni.
 
Ni kiduka kidogo. Na sio frem bali kibanda cha chuma. Majirani zangu nafikiri wanalaza zaidi ya 500K kutokana na kuwa na wateja wengi sana sababu wamekaa miaka mingi sana hapa.
Dah kumbe hii biashara inalipa Kama ndio kweli iko hivyo Kama ulivyoeleza ndugu.
Na je katika mauzo ya laki 2 hapo faida yako inaweza kuwa shilingi ngapi?
 
Dah kumbe hii biashara inalipa Kama ndio kweli iko hivyo Kama ulivyoeleza ndugu.
Na je katika mauzo ya laki 2 hapo faida yako inaweza kuwa shilingi ngapi?
Kwa uzoefu wangi faida ni ya kudunduliza mfano kiroba unga unaweza kua na faida ya 5000 unauza siku 2.....sukari ina faida ya 9000 unauza siku 4..... Dumu La mafuta lina faida ya 13000 unauza week 1 so ndo faida ilivyo...

Bidhaa zinazouzika sana faida hua ndogo mfano vocha viberiti sabuni na mikate na ukiona bidhaa unanunua 7,000 ukiuza unaopata faida ya 25000 unaweza kuiuza kwa mwezi mzima.
 
Duu mkuu unanunua wapi unga na sukari? uku kwetu unga Kg 25 ni 27elf na sukar kg 25 ni 55elf rejareja unga kilo 1200 na sukari kilo 2500.
 
Faida ni asilimia 10 , ukiuza laki na ukachukua 20000 , ujue umechukua 10000 ya mtaji. Likifa duka usilaumu, kwani umegeuka kuwa chuma ulete wa duka lako
Si kweli.. Mimi kila bidhaa nayoingiza dukani lazima nijue INA asilimia ngapi ya faida.. Na nyingi ni 20% na kuendelea na nyingine zinafika mpaka 200%
 
Mimi nlifunguliwa mwaka jana nikala mtaji likafa, sasa hivi nina biashara ingine kabisa rafiki yangu alinshauri nifungue supermarket nikamjibu hapana nahitaji biashara itakayonipa kwa siku faida ya zaidi ya 35% per day, hata ikiwa seasonal business ila ya dizaini hiyo hapana maana mimi mwenyewe mtumiaji mzuri sana wa pesa nkijiskia hamu ya kula kuku choma napita bodaboda anafata sasa biashara kama hizo ukitoa 20,000 au 30,000 kwa matumizi binafsi unakula mtaji, ndo nililojifunza hapo.
 
Dah kumbe hii biashara inalipa Kama ndio kweli iko hivyo Kama ulivyoeleza ndugu.
Na je katika mauzo ya laki 2 hapo faida yako inaweza kuwa shilingi ngapi?
Hii biashara inalipa, japo wengi huiponda. Ni kuwa mbahiri tu. Mfano, maharage ya njano quality unanunua 1800 na kuuza 2400 kilo na hayakai, mchele unanunua 1700 au 1600, unauza 2, 000 kama upo location nzuri ni angalau sku 10 umemaliza kilo 100. Sukari unanunua 108,000 unauza 2500 na kupata 125,000. Kufuli ya kuuza 3500 unainunua 2000 au kasoro bei ya jumla. Taa ya kuuza 2500 unainunua 1700,.. n. K. Japo zipo bidhaa ambazo faida haifiki hata sh. 50.

Kama nilivyosema awali mi huwa sicomplicate kupiga mahesabu eti nimeuza labda 150K then faida ni kiasi gani. Nimejiwekea tu nipate elf 20 kila siku.
 
Kwa uzoefu wangi faida ni ya kudunduliza mfano kiroba unga unaweza kua na faida ya 5000 unauza siku 2.....sukari ina faida ya 9000 unauza siku 4..... Dumu La mafuta lina faida ya 13000 unauza week 1 so ndo faida ilivyo...

Bidhaa zinazouzika sana faida hua ndogo mfano vocha viberiti sabuni na mikate na ukiona bidhaa unanunua 7,000 ukiuza unaopata faida ya 25000 unaweza kuiuza kwa mwezi mzima.
Ni kweli mkuu, lakini hapo ndo linakuja suala la kuchagua location nzuri. Mfano ukiwa eneo lenye mama ntilie na wapika chips dumu la mafuta linaisha siku 2 au hata 1 wakat mwingine, maharage, mchele havikai. Unadunduliza lakin vikiwa na speed ya kutoka huumii sana
 
Faida ni asilimia 10 , ukiuza laki na ukachukua 20000 , ujue umechukua 10000 ya mtaji. Likifa duka usilaumu, kwani umegeuka kuwa chuma ulete wa duka lako
Hiyo hesabu ya 10% umeipata vipi mkuu? Huwa haina ukweli wowote hiyo, vinginevyo ningekuwa nshafilisika au biashara ingekuwa haikui
 
Pitia hapa. Hutakosa kuokota a thing or two.
 
Attachments

Mimi nlifunguliwa mwaka jana nikala mtaji likafa, sasa hivi nina biashara ingine kabisa rafiki yangu alinshauri nifungue supermarket nikamjibu hapana nahitaji biashara itakayonipa kwa siku faida ya zaidi ya 35% per day, hata ikiwa seasonal business ila ya dizaini hiyo hapana maana mimi mwenyewe mtumiaji mzuri sana wa pesa nkijiskia hamu ya kula kuku choma napita bodaboda anafata sasa biashara kama hizo ukitoa 20,000 au 30,000 kwa matumizi binafsi unakula mtaji, ndo nililojifunza hapo.
Hii biashara inataka ubairi sana. Ikibidi unapiga hata mlo mmoja siku inapita
 
Af kuuza lak 1 sio maeneo yte..Kuna maeneo mengne hata elfu 20 ni mbinde
 
Wakati huo huo kuna mwingine anauza hadi laki 7 kwa siku. Kuna watu wanauza acha kabisa, hasa waliopo karibu na vituo vya daladala mfano pale Kimara Korogwe, Mbezi, etc.
Af kuuza lak 1 sio maeneo yte..Kuna maeneo mengne hata elfu 20 ni mbinde
 
Back
Top Bottom