Kina nani hawakupinga misaada ya kigeni kabla ili kutaka kujitegemea?

CHALLENGE
MM
Njoo uishi Tanzania isiyopokea misaada kwa mwaka mmoja tuu
Njoo wakati tunavumilia maumivu ya kuwacha ulevi wa kutegemea misaada
Hata teja anapewa methadone ili awache uraibu taratibu
Oh..by the way pitia Sumbawanga/Tunduma,Tanga/Horohoro,Namtumbo/Mbinga uwambie tulifanya makosa kupokea msaada wa MCC kuwajengea barabara hizo
 
Hilo ndio tatizo; kwa hiyo kama Uchaguzi wa Zanzibar usingefutwa na Shein angeshinda kihalali bado watu mngeendelea kutaka misaada?
mkuu tuelewane kdg..hata mimi napenda tanzania tuache habar ya misaada ili tujenge msingi mzuri wa kujitegemea na kuondo foreign influence kwe mambo yetu..ila mi nashangaa watu wanataka kuficha sababu ya sisi kusitishiwa misaada ni nini badala yake wanadandia ooh inabidi tujitegemee misaada haina maana..kabla hatujafika huko kwanza tumezikosa hz pesa kwasababu ya mambo yaliotajwa.......tuache misaada sawa ila sio tusitishiwe misaada kwa vikashfa flan tutofautishe hapo mkuu..haijalishi rais ni nani..lets say yalitokea lets say tusitishiwe misaada kisa yalitokea mauaji ya halaiki halafu c tujisifu eti hatutaki kuwa tegemezi noo...km tumeamua kutopokea hapo sawa ila sio tusipokee kisa tumepiga blanda flani
 

Does this justify what happened in Zanzibar?
By the way even if you think MCC is a dead clock,but even the dead clock is right twice a day, One of the moment where MCC is right is on this sham elections in Zanzibar!
 

Lakini, nimeonesha kuwa mimi suala la misaada kupinga halijaja na hili la MCC wala Zanzibar. Binafsi yaliyotokea Zanzibar nikiamua kuyaongelewa nitazua kashfa nyingine ndio maana ninakwepa tu kw amakusudi. Binafsi sipendi misaada ya kigeni kwa sababu yoyote; na haijalishi wao wanasema kwanini wamesitishwa. Tatizo ni kuwa kwa vile wanasema ndio sababu basi na wengine wanaamini kabisa kuwa ndio sababu.
 
Does this justify what happened in Zanzibar?
By the way even if you think MCC is a dead clock,but even the dead clock is right twice a day, One of the moment where MCC is right is on this sham elections in Zanzibar!

What happened in Zanzibar? Kilichotokea Zanzibar ni siasa za Zanzibar period. Irrelevant and inconsequential. Mtanitafuta ugomvi bure tu. Zanzibar walitaka kuiba uchaguzi kwa kulazimisha kushinda wakachomolewa kama walivyotaka kujaribu Bara wakawahiwa. Simple as that.
 
Hilo ndio tatizo; kwa hiyo kama Uchaguzi wa Zanzibar usingefutwa na Shein angeshinda kihalali bado watu mngeendelea kutaka misaada?
Mzee Mwanakijiji mbona unakimbilia kujibu coment ambazo hazina mijadala tunayoitaka hapa!!?? Hebu rudi ujibu hoja ya Gamba la Nyoka post number #6. Halafu hatuna tatizo na mabandiko yako kuhusu suala la misaada,lkn unaweza kurejea pia mabandiko yako yaliyohusu cyber crime!!?
 
Mimi nimekuwa nikipinga misaada kwa muda mrefu sana sasa.

Kuna wakati huwa nafikia sehemu nadhani labda niko peke yangu tu kwenye kupinga hilo.
Ni kweli misaada hatuitaki, na demokrasia na uhuru wa kutoa habari hatuutaki pia?
 
hapo ni sawa mkuu......unajua watu wanadiscuss umuhimu wa kutotegemea misaad ya manchi mengine af kuna watu kama umewaona wanataka kutumia discussion hio kufunika issue ya zenji hao ndo wananiboa mkuu..pamoja sana
 
Watu wanatakiwa kufahamu every decision in life has consequences, ts the way you handle them is what determines that are positive or negative, na hata tungeendelea na misaada bado changamoto zungekuepo na bado tunazuona so lets try the other side, hongera sana mzee mwanakijiji kwa kuainisha haya mambo nani lazima watu tuelewe tusikariri kukariri
 

Magode, tatizo langu la cybercrime ni kuwa nilikuwa wa kwanza kuwaonya wapinzani na wapenda demokrasia juu ya ujio wa sheria hii tangu baada ya uchaguzi wa 2010. Wakati wengine walikuwa wanaishi katika kufurahia kupendwa na kukubalika wengine tulishajua kuwa CCM walikuwa wanaenda kufanya nini wakati ule ili wasiende kwenye uchaguzi mkuu wa 2015 katika mazingira yale yale. Ndio maana wakati wengine wanashtuka baada ya kuja kwa Cybercrime Bill wengine tulishaachana nayo kwani itakuwa ni kudandia tu wakati tulishapiga kelele juu ya hilo. Ukitafuta kunisoma unaweza. ila kwa vile unaweza kufikiria labda sijawahi kuzungumzia rejea hapa:

Niliandika:
Here we go.... Tanzania new internet policy...Activists and online journalists beware

Niliandika hilo Nov 24, 2012. Na ukitaka kujua nilichokisoma angalia "my take" niliyoandika humo. Siyo watu waliokuja kushtuka miaka mitatu baadaye! Sidhani kama utarudi na kukiri nilikuwa sahihi na mbele ya wengine ambao leo wanatutuhumu wengine ati hatujazungumzia mambo haya. Wanasema sisi ndio tumebadilika!
 

Mkuu mwanakijiji nakubaliana sana na wewe, nadhani kwenye post yangu asubuhi niliomba uje hapa nyumbani utupe ujuzi uliochuma huko nje, hizi nadharia kwetu imegeuka kuwa tatizo. Wenzetu wachina walienda kwenye nchi za watu wenye techology ya juu wakajifunza wakarudi kwao kufanyia kazi waliyojifunza, wewe kimekushinda nini? Nilitoa na mfano wa wahadhiri wa vyuo vyetu wanaosema watu wafikiri ili kujikwamua kimaisha lakini wenyewe ukiwatoa kwenye ajira wanageuka kuwa maskini. Kama ni kweli wewe unapinga sisi kupewa misaada kwanini usije nchini utusaidie na mawazo yako nini kifanyike ili tutoke hapa tulipo? Juzi kuna kituko kimetokea mkuu wa mkoa fulani baaada ya mabadiliko akakosa cheo huku ana Phd lakini jinsi alivyoomba kila mtu ameshangaa. Lakini ungefanikiwa kumsikia akiwa madarakani ni kulaani watu wasiopenda kazi wala kujituma. Wewe kinakushinda nini kurudi nyumbani wakati unaona sisi tunataka kushikishwa ukuta na wazungu? Njoo kwenye uhondo wa ngoma sio kuwa mshauri mzuri kinadharia wakati uwanja uko wazi. Njoo nyumbani tuone huo umahiri wako wa kuona makosa ya wengine uwanjani na jinsi ya kuyarekebisha ukiwa jukwaani.
 
Kwa hoja hizi nzito...lazima watumie multiple IDs kutukana na kuondoa hasira zao,hoja kimsingi iko wazi.Kuna watu wanaongelea suala la Zanzibar kipropaganda....ili kuhalalisha uovu waliopanga na serikali za magharibi..lilikuwa ni jaribio kubwa kwa usalama wa Tanzania....lazima tuseme ukweli pia hata hizo ahadi za wahisani hazijawahi kutimizwa asilimia 100 na wanapokumbwa na ukata hutowa sababu kama hizi kuficha aibu yao hata kama umetimiza vigezo.
 
Hamna ushahidi duniani uliothibitisha misaada na kuomba hukuza uchumi,je wao hupata nini kwa kutowa?...Kuna kitabu kinaitwa Dead Aid by Dambisa Moyo (Mzambia),pia kwenye youtube kuna debate akiwa na wasomi wa kizungu akitowa hoja zake kuthibitisha madhara ya misaada ya kudumu kwa Afrika,waweza kufuatilia.
 

Kweli unachosema? halafu hizo asilimia chache zilipofika hapa nchini zilitumika vizuri kwa asilimia 100? Acheni utani basi jamani. Wenye shida ya hizo hela ni sisi na wala sio hao waliotunyima, utasikia propaganda za kichovu eti wapemba watawarudisha waarabu, lakini wakati huohuo raslimali karibu zote zinasimamiwa na kuvunwa na wageni sisi tunaishia kupewa mirahaba ya chini mno. Ukiangalia hao waarabu wako wangapi na huo ukubwa wa pemba ni kiasi gani mpaka leo tuogope waarabu unabaki kinywa wazi. Hao akina mwanakijiji wamebaki na minadharia tu huko nje lakini hawako tayari kuja hapa nyumbani kuonyesha ni jinsi gani tuone anaweza kulisaidia taifa.
 
Waarabu na wapemba umeongea wewe,jikite kwenye mada ili tupate suluhisho.
 
WanaCCM tumeshaeleza wazi kuwa hatuna shida na vijimisaada vyenye masharti. Hili hata mstaafu Kikwete alilizungumza na sasa rais Dkt Magufuli anazidi kulikazia.

Hebu sema kweli mmesema lini na wapi? Je, unafikiri hilo linafanyika kwa sababu za kusema tu?

Tatizo nyie wana CCM na huyu Mzee Mwanakijiji mnadhani sisi wengine tunaowashangaa mnadhani tunaikataa dhana ya kujitegemea na pengine hatupendi kujitegemea.

La hasha ndugu!!

Hivi mtu anawezaje kutokuwa tegemezi iwapo anashindwa hata kujisimamia kwa kufuata taratibu alizojiwekea yeye mwenyewe mpaka uamushwe toka uzingizini na mtu mwingine, kwamba, wewe vipi....umelala umepitiliza .....amka!!??

Halafu tunachotofautiana na kupingana nanyi, actually, si nia ya kupenda na kutaka kwetu kujitegemea isipokuwa tunapinga kivuli mlichotuzibia mbele nyie wana CCM hata tusione njia ya kuelekea kwenye kujitegemea na wakati huohuo mnatuhimiza na kutuimbia nyimbo tamutamu za "...oh tunatembea na si muda mrefu tunafika ktk mji ule mtakatifu wa kujitegemea!!"

Yaani ni unafiki kwa kwenda mbele!!
 
Waarabu na wapemba umeongea wewe,jikite kwenye mada ili tupate suluhisho.

Suluhisho ni rahisi sana, ni kutimiza demokrasia kama inavyopaswa na iwapo utashindwa ni lazima ukubali. Na iwapo tuna lengo kabisa la kutoka hapa tulipo ni lazima tukope ili kukuza kilimo na kujenga viwanda vya kutosha. Kinyume na hapo tutashinda hapa kila siku kulaumiana na wale wengine kupambana kuhakikisha wanasifiwa bila kuleta maendeleo zaidi ya kubaki madarakani.
 

Utashangaa wanaohubiri kujitegemea wanaoana sifa kutumia bidhaa za nchi za nje hata zile zinazopatikana hapa nchini. Kituko kikubwa wote wanaohubiri kujitegemea ni wale wenye ajira au nafasi kwenye serekali, sasa watoe kwenye hayo madaraka au ajira uone wanavyochanganyikiwa. Watu tunapenda sana kujitegemea kwani mpaka sasa hatuna nafasi zozote katika serekali bali ni wajasiriamali tunaopambana kwa kila hali. Ila tulichogundua serekali haina taarifa na wakulima ambao ndio wengi kwani viongozi wengi maendeleo na kujitegemea, wanayaongelea kinadharia zaidi kuliko uhalisia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…