Heshima kuu Mwanakijiji,
ndani ya jamvi hivi tuna uelewa tofauti nami binafsi kuna thread nashindwa kufuatilia kwa kuwa nahisi si level yangu.
Mwanakijiji ulikuwa role model wetu humu ndani lakini naona kwa sasa unaelekea kupungukiwa na uwezo wa kusimamia ukweli.
MCC wamesitisha msaada kwa Tanzania na sababu wamezitoa,ningetegemea tungejikita katika kuona sababu walizotoa MCC kuwa na sawa au wamekosea.Kwa mfano tungetetea uchaguzi wa marudio kwa vifungu vya sharia na reference kwa case zingine.Pia cybercrime tungeeleza na kufafanua kwa kina hii ingesaidia wote kuwa wamoja kama inavyokuwa kwa Myahudi anapokabiliana na Mpalestina.
Kwa uwezo wako wa kudadisi ungeweza hata kutusaidia kuhusu hili la iwe iweje SEIF hawezi kutawaka Zanzibar kwani binafsi nahisi viongozi wetu kuna jambo kubwa wanalijua kuhusu SEIF lakini hawatueleze na inatufanya tuendelee ku sympathisize na SEIF.
Mwanakijiji naamini unakumbuka Mwalimu alivyojitahidi kupingana na mashirika ya fedha ya kimataifa na naamini pia unakumbuka nchi hii ilifikia hata nguo kukosekana,ulanguzi,sukari na unga wa foleni,maduka ya RTC.Hatuna la kujifunza kweli?