pastorletta
Senior Member
- Jan 9, 2011
- 195
- 121
Hoja siyo kuwa na misaada ya kigeni au kutokuwa nayo. Ni wazo zuri kujitegemea ndiyo maana chama kilichopo madarakani kilipoondoa Azimio la Arusha kinyemela - Azimio lililofafanua hatua kwa hatua tunavyoweza kuwa taifa linalojitegemea, wenye uoni wa mbali walipiga kelele. Hatuna sababu ya kuwa wategemezi wakati tuna hazina kubwa ya utajiri. Vietnam walikuja hapa kujifunza kilimo cha Korosho wametuacha. Nchi tulizopigania kuzikomboa kisiasa zimetuacha kiuchumi. Hapa kuna tatizo la uongozi na siasa safi. Watu na ardhi tunavyo. Kinachoshangaza ni pale mtu anapokosa siasa safi (ya kidemokrasia) na mikakati sahihi ya kuitoa nchi katika umaskini (uongozi bora) na kisha kuadhibiwa kwa kukosa vitu hivyo, na kuanza na badala ya kujisahihisha kudhani kuwa atatumia mwanya huo kutushawishi tusitegemee misaada ya nje. Tunapoangalia uwezekano wa kujitegemea (si kwa hasira kwa kuwa tumenyimwa misaada kwa sababu ambazo zingezuilika), tujitathmini tutaendeleza aina hii ya utawala usiozingatia sheria kwa maslahi ya nani? Hakuna ubaya wowote kujielekeza katika kujitegemea huku tukidumisha mahusiano mazuri na waliopiga hatua za maendeleo na tukijisahihisha kwa tabia zinazoonwa na wenzetu na zinazolalamikiwa na watu wetu kuwa si za kistaarabu. Tusifumbie macho ukweli.