lakini yote tisa nachojua Mbeya na hasa huko wilaya yao hawa jamaa kuna matatizo makubwa sana ya Ukabila kiasi kwamba sio swala la Mtandao ama elimu zao bali kabila lako... kumbukeni hawa jamaa wamesoma karibu wote ktk vinyang'anyiro vya uongozi. Na tukumbuke kuwa Mwandosya ktk pita zake zote toka huko nyuma Mtandao never existed ila tumekuja yajua haya yote mwaka 2005 tena basi Sam original ndiye alotupa majina ya wahusika.
Wilaya ya hawa wagombea wawili imegawanywa kiasi kwamba kuna wabunge wawili (Prof. Mwandosya - Rungwe mashariki na Prof. Mwakyusa- Rungwe magharibi),hivyo tusianze kuzua hapa kwamba Mwandosya kenda msaidia Mwakyusa ktk chaguzi za Ubunge. Wote wamekuwa na wakati mgumu sana inapofikia swala la kabila. Kifupi ktk mikoa yote pamoja na kwamba Mbeya ni CCM damu kuna matatizo makubwa ktk teuzi zao.
kwa sababu naelewa kuwa watanzania ni wepesi wa kusahau nitawakumbusha tena, Mwandosya na Mwakyusa wote wamepita mara zote kwa mapendekezo makubwa toka uongozi wa juu wa chama CCM, na kuondoa ubishi huu nadhani maelezo haya yata prove nilichosema:-
http://www.kikweteshein.com/habari/articles/66/1/Nawataka-maprofesa-hawa%2C-nipeni%2C-nitawatumia
Mkandara,
Inaelekea hujui kabisa Geography ya mkoa wa Mbeya. Wacha nikueleweshe, Wilaya ya Rungwe na Kyela zina Wanyakyusa karibu asilimia 100. Kwa maana hiyo kwenye hizo wilaya ukabila sio tatizo kwasababu karibu wote ni kabila moja. Kila atakayegombea
cheo chochote toka chama chochote most likely atakuwa Mnyakyusa.
Kyela ina watu waliohamia toka Ruvuma miaka mingi ya nyuma, kule wanaitwa Wakisi, hawa ni wachache sana na hawazidi hata asilimia 5.
Ileje ina Wandali kwa asilimia kubwa ingawaje kuna Wanyakyusa wachache sana, kiujumla viongozi karibu wote wanaotoka huko ni Wandali.
Tatizo la ukabila liko Mbeya mjini ambako kuna makabila mawili makubwa, Wanyakyusa na Wasafwa, pia kwasababu hapo ni mkoani basi kuna makabila mengine mengi pia. Hapo ndio kunakuwa na mambo ya ukabila wakati wa kampeni. Hicho sio kitu cha ajabu maana kinatokea hata sehemu nyingine.
Kama ni ukabila mwondoe kabisa Prof. Mwandosya kwenye hilo, yuko kama Watanzania wengine ambao wanaheshimu makabila yao lakini haya affect maamuzi yao.
Kumbuka mwaka huu CCM wamechagua mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya ambaye sio Mnyakyusa wala Msafwa. Hii ni dalili siasa za mkoa ni zaidi ya ukabila. Halafu suala la Mwang'onda Na Mwandosya wote ni Wanyakyusa, tofauti tu mmoja ni wa kuzaliwa huko Mbeya wakati mwingine wazazi wake wamekulia nafikiri Tabora.
Inaelekea Mkandara habari ulizonazo kuhusu prof. sio sahihi kabisa. Hata link uliyotoa hailezi chochote kwamba prof. Mwandosya alikuwa na matatizo ya uchaguzi Mbeya. Sijui tume ya uchaguzi lini ilitangaza watu waliopita bila kupingwa ila nahisi
wakati huo JK anapita Mbeya, tayari prof. Mwandosya alikuwa ni mbunge mteule baada ya kupita bila kupingwa au ilikuwa siku chache kabla ya tume ya uchaguzi kumtangaza kwamba kuwa mbunge mteule.
Nakutumia link nyingine ya CCM na matokeo ya Wabunge, jina na
wilaya ya Prof. Mwandosya havimo kwasababu alipita bila kupingwa.
Hakukuwa na uchaguzi wa ubunge kwenye jimbo la Rungwe Mashariki. Ni sawa na ambavyo Lowassa alipita bila kupingwa kule kwao. Tofauti tu ni kwamba Prof. kapita bila kupingwa mara mbili zote.
http://www.ccmtz.org/ubungej.htm
Pia angalia kura za prof Mwakyusa, katika mkoa wa Mbeya upande wa CCM, yeye ndiye alipata asilimia ndogo ya kura kuliko wabunge wengine wa CCM? Why? mimi sijui, ninachojua tu ni kwamba 2005 alijitahidi sana maana mwaka 2000 aliponea chupu chupu, alimpita mpinzani wake kwa kura chache mno pamoja na prof. Mwandosya kutumia muda wake wote kumsaidia. Bado ninadhani 2010 kwa prof. Mwakyusa kutakuwa na ngoma nzito kule jimboni kwake. Si unajua hata kwenye uchaguzi wa CCM wilaya ya Rungwe mwaka huu, alizomewa na wananchi walikataa yeye kuwa msimamizi wa uchaguzi?