Kina nani watahesabiwa siku ya sensa?

Kina nani watahesabiwa siku ya sensa?

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
204
Reaction score
231
Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), katika siku ya sensa watu wote watakaokuwa wamelala nchini watahesabiwa. Hawa watahesabiwa katika kaya na jumuiya kama hotelini, nyumba za wageni, hospitalini, magerezani, mabwenini na kwingine wanakojumuika watu wengi.

Vilevile watahesabiwa watakaokuwa kwenye kambi za kijeshi, vituo vya kulelea watu wenye mahitaji maalumu, wakiwamo yatima, wazee na kambi za wavuvi, watu wasio na makazi maalumu, vituo vya usafiri wa umma kama stendi, viwanja vya ndege, bandari, vituo vya treni na huko kutakuwa na utaratibu maalumu.

Ili kuhakikisha jambo hilo la taifa linafanikiwa, tayari makarani wameandaliwa vema na wana maswali watakayouliza.
 
Back
Top Bottom