Ni wazi kuna ufisadi tayari umefanyika chadema makao makuu taifa. Lakini pia ni wazi kwamba kuna matumizi mabaya ya ofisi, matumizi mabaya ya madaraka, matumizi mabaya ya rasilimali na fedha za chama yasiyofuata, wala kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na katiba ya chama hicho, yanaendelea kufanyika ndani ya chama hicho kilichokua kinapitia ukata mkubwa sana wa fedha kwa muda mrefu.
Licha ya viongozi wa kitaifa wanaotuhumiwa kwa ufisadi huo kutumia mitandao ya kijamii na kuwatumia vijana wa chama, kutetea ufisadi wao na kuwakingia kifua kwa kurusha lawama kwa wengine ili kuficha au kukwepa tuhuma hizo za ufisadi, matumizi mabaya ya ofisi, madaraka, rasilimali na fedha na fedha za chadema kwa manufaa binafsi, bado hakuna kinachoweza kukinusuru chama hicho kupata hati chafu au yenye mashaka kwasababu ya ufisadi ulioibuliwa.
Kama mdau wa jukwaa hili la siasa jf, unashauri chadema wafanye nini kujikwamua kutokana na mkwamo huu wa kifisadi unaowazonga na kuwafedhehesha mbele ya umma?
Ni upi mwisho wa sakata hili la kifisadi ndani ya chadema makao makuu?🐒
Mungu Ibariki Tanzania