Uchaguzi 2020 Kinachoendelea Kampeni za CHADEMA mwaka huu 2020

Uchaguzi 2020 Kinachoendelea Kampeni za CHADEMA mwaka huu 2020

Sungudi

Member
Joined
Aug 6, 2014
Posts
48
Reaction score
35
Ndugu WANA FORUM,
Kampeni za chadema mwaka huu hazina ile amsha amsha tulioyozoea miaka ya nyuma.
Naona viongozi wote wa kitaifa na wagombea wote wa kitaifa wanafuatana kwa pamoja mfano pale shinyanya Alikuwepo M/kiti, mgombea urais na makamu. Je haiwezekani kugawana pa kwenda? Kuna ulazima wa kuwa pamoja kama ny*mbu?
Kuna haja gani ya kushukia mjini kahama kwa ndege then unasafiri kwa gari zaidi ya km 100 kwenda shinyanga na kuacha kuto- kuwasalimu wana Kahama? Ilishindikana nini kuwahi kidogo angalau afanye mkutano mmoja kahama then jioni (kama walivyofanya) waendelee na mkutano Shinyanga? Je hii ni dharau kwa wana kahama? Ni matumizi mabaya ya rasilimali za kampeni? Au ni kutojipanga?

Pili nimegundua tangu wawatimue TBC kama vile wamesusiwa na media ama kuna mgomo baridi. Kile kitendo kimewaharibia sana picha kwa jamii ya wanahabari. Kama media house kubwa TBC anafanyiwa vile nani atathubutu kufanya kazi na hiki chama? Kama mpiga picha anadhalilishwa na kuhatarisaha maisha yake kwa tuhuma ambazo kimsingi sio zake ni za mrusha matangazo aliyepo studio, ni mwandishi yupi anaweza kuhatarisha maisha yake?Ningeshauri Waombe msamaha na kuahidi kutorudia hili jambo, ili twende pamoja na waandishi na media!
Sera!
Hawanadi sana Sera zaidi ya kutumia nguvu nyingi kuonesha wao sio vibaraka wa mabeberu. Wangenadi zaidi Sera na ilani yao, automatically wangekuwa wameonesha namna walivyodhamiria kuendeleza nchi na mwananchi. Hii ingetosha zaidi. Lakini ndugu Lssu mpaka sasa hivi anazidi kuharibu maana anasema hata makinikia sio yetu hatuna haki nayo... Anazidi kuharibu...

Karibuni na nyie wadau mchangie namna wanavyoharibu ili wajirekebishe mapema
La sivyo Act watanyakua nafasi ya CDM na kuwa KUB!

Wasalaam!
Sungudi!
 
Mara amsha amsha hamna, mara unatembea 100km bila kusimama!! Wewe unachotoka ni nini haswa? Na kwa nini upange ratiba isiyokuhusu?

Pambana na hali yenu.
 
kila siku mnaandika marudio tu mbona mnateseka si mchambue vyama vngne cdm inawakosesha raha😀😀😀😀
 
Hahaha TBC ni ccm, TCRA ni ccm, tume ya uchaguzi ni ccm, wataipendaje CHADEMA?!
 
Hahaha ACT hawajawafukuza TBC uliona wanavyokata hotuba zao, angalia za Magufuli linganisha na za Membe
 
kila siku mnaandika marudio tu mbona mnateseka si mchambue vyama vngne cdm inawakosesha raha[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Penye makosa wajirekebishe.
Pale Tinde alipita Magu... Akakusanya nyomi la ajabu.. Yeye Liss kapita hapo mbio.. Hataki kura za Tinde? Achilia mbali za huko kahama aliposhukia na ndege! Amepita miji midogo yote mfano Isaka na kagongwa... Anaumiza wakereketwa!!!!!!!!
 
Kwanini unataka kila kitu kifanane na jana? Mazingira hayafanani kulingana na mahitaji ya nyakati hivyo huwezi kufanya kitu kilekile na ukategemea matokeo tofauti
 
Kwamba sio lazima waende pamoja kama Nyumbu,,!!!.
Kampeni zanahitaji pesa, na pesa kwasasa Chadema hawana kabisa, pesa ya kufanya mashambulizi ya kampeni kama zamani mgombea mwenza awe kusini alafu mgombea urais awe Lake Zone.pesa zote kaficha Mbowe.
 
Kwamba sio lazima waende pamoja kama Nyumbu,,!!!.
Kampeni zanahitaji pesa na pesa kwasasa Chadema hawana kabisa.pesa zote kaficha Mbowe.
Sasa kweli ufike kahama, Isaka, Tinde na miji kibao njian tena mpo wote uachane nao.. Ukimbilie shinyanga!!!
Kw a taarifa huko kahama kuna makamanda wengi sana amewaangushaà...
Tahadhari wasijee piga za kulipiza kisasi kwa kudharauliwa? Kulikuwa na gharama gani kusimama hayo maeneo?
 
Tinde alikusanya nyomi akiwa anakwenda wapi?
Penye makosa wajirekebishe.
Pale Tinde alipita Magu... Akakusanya nyomi la ajabu.. Yeye Liss kapita hapo mbio.. Hataki kura za Tinde? Achilia mbali za huko kahama aliposhukia na ndege! Amepita miji midogo yote mfano Isaka na kagongwa... Anaumiza wakereketwa!!!!!!!!
 
Inavyo semwa Uhuru wa habari hakuna hata hao waandishi wameona wamenusurika wao na vyombo vyao zidi ya tisiarei na Sheria ya habari ambayo ni mwiba mkali kwao.
 
CDM sikio la kufa hao, leo wapo Tabora hutaoni picha hadi zipitie kwa mhariri wao azitengeneze ndio warushe, hawa jamaa watakata tamaa hata kabla ya kumaliza kampeni, hapa wanasubiri mkutano wa Mbeya ndio watume picha chache na vi clip vya dk 2.
 
Sasa kweli ufike kahama, Isaka, Tinde na miji kibao njian tena mpo wote uachane nao.. Ukimbilie shinyanga!!!
Kw a taarifa huko kahama kuna makamanda wengi sana amewaangushaà...
Tahadhari wasijee piga za kulipiza kisasi kwa kudharauliwa? Kulikuwa na gharama gani kusimama hayo maeneo?
Jamani ratiba imesema mkutano ni shinyanga ila magufuli hiyo mikutano ipo kwa ratiba.

Chadema hapa wanamtambulisha kwa kanda zote basi sio mikutano ya jimbo kwa jimbo bado haijaanza.

Ratiba ya NEC ipo humu kabla hamjaanza kujifanya wachambuzi isomeni.
 
CDM sikio la kufa hao, leo wapo Tabora hutaoni picha hadi zipitie kwa mhariri wao azitengeneze ndio warushe, hawa jamaa watakata tamaa hata kabla ya kumaliza kampeni, hapa wanasubiri mkutano wa Mbeya ndio watume picha chache na vi clip vya dk 2.
Umeonae?
 
Back
Top Bottom