Fedha za mambo ya ovyo ovyo zipo siyo za maendeleo ya watu. Kwa mfano badala ya kuwekeza gharama kubwa ya kununua magari ya washa washa kuwaumizia raia wako unge nunua matrecta na kuwakopesha kwenye viji na kuhakikisha wakulima wanapata huduma kwa bei Raisi kwa mfano heka moja ukalimiwa kkwa sh. 20,000 badala ya 50,000 mpaka 70,000 na vijana wengi wakapata ajira uhalifu ungepungua na nchi ingekuwa na uhakika wa Amani. Ona sasa kinachotokea Conga, serikali imeuwa vijana 170 hadharani laana inakuja vijana hao wanataka kuing'oa serikali madarakani wakisaidiana na M23. Pamoja wale vijana walio uliwa wengi wao walikuwa ni wahalifu waliokubuhu lakini wamefika ktk hatua ile ni baada ya misingi ya nchi kusahau sera za vijana. Kwa mfano kupatikana kwa vitabu mashuleni, Kujengwa kwa wingi vyuo vya ufundi, Mikopo yenye Riba na masharti nafuu.Sasa usipotimiza hayo halafu ukaseme vijana wajiajiri watajiajiri kwa skils zipi zaidi ya kuwa vibaka. Serikali inatakiwa iweke miundo mbinu wezeshi kwa vijana kupata elimu pamoja na ujuzi wakuweza kujitegemea. Kunakipindi fulani kulikuwa na wimbi kubwa la vijana wakitanzania kuzamia Meli, ingawa sasa limepungua, kukaja wimbi la vijana wengi wa Kitanzani kwenda kwa nia haramu Afrka kusini, ingawa kwa sasa nalo limepungua, hivi sawa wimbi kubwa la vijana nikujishughurisha na umachinga ktk sehemu zisizo rasmi kwahiyo kunakamata kamata kila siku huko mijini. Kilimo peke yake ndicho kitakacho weza kumuokoa kijana wakitanzania kwa sasa. Tuna ardhi kubwa sana na yenye rutuba bidhaa za kilimo zinahitajika sana duniani yakitengwa maeneo Rasmi kwa ajili ya kilimo cha biashara yakapimwa vizuri alafu wakagawiwa vijana.Ikatengwa bajeti ya kuwakopesha ili waendeleze hayo maeneo mkopo ukawa wa mda mrefu tena wangeanza na wanafunzi wa Sua wanao maliza degree na Masters baada ya hapo.serkali ikipata uzoefu wa uendeshaji wanashuka hata kwa vijana wasio na Elimu, hii migrant from vijijini kuna mjini ingeisha kabisa. Ila serikali yetu inaweza zaidi ktk kujilinda ili wapizani wasiiwanyang'anye madaraka. Ni kweli unaweza ukawadhibiti wapinzani au ukawamaliza nguvu kabisa na wakafutika wenyewe, Ila wananchi huwezi kuwadhibiti hayo yanayoendelea Congo ni matunda yalio Anzia kwa Rais Mabutu sasa madhara yake ndiyo hayo yanayoonekana Leo. Tanzania tusipoangalia tutafikia huko. Chama kinaweza kikawa hata kimoja ila kama kitaweza kuendesha nchi kwa misingi iliyo sawa na haki wananchi wake hawana shida nacho, lakini ukiona malalamiko kila kona ujue kuna udhaifu mahali. Watu wanasema oooh kwakuwa Rais ni MwNamke kwa hiyo watu hawamuogopi. Uraisi ni taasisi na taasisi haina jinsia kikubwa ni mifumo ya nchi ipoje. Nakomea hapo kwanza kwa leo. Watanzania wote tunapaswa kuijenga nchi yetu kwa mioyo yetu yote. Na wale wanaotapanya Rasilimali zetu tusiwaonee aibu tuwakemee, kwani hizi rasilimaliinakwenda zikiisha hasa rasilimali asili