Huu uchaguzi mdogo umefungua mengi na wale ambao wanafanya mikakati ya Chama au strategist wa CCM wamekosea sana. Wamecheza karata kwa kuonyesha kadi zao na kwa msingi huu wapinzani siku zijazo chache watatangaza kutokushiriki uchaguzi wa 2020 mpaka kuundwe tume huru ya uchaguzi. Wale ambao wanafurahia hili ya kata wamepewa kazi sasa ya kushika viazi vya moto. Nchi yetu kwa sasa inaingia kwenye mgogoro mkubwa sana wa kisiasa ambao haujawahi kutokea. Wale wanaofikiria watawabeba beba watu tu wamekosea. Tujifunze kutoka Kenya wakati wa uchaguzi biashara zinagugwa kwa uoga na wawekezaji wanasimamisha uwekezaji kwa hadi miaka miwili mwaka wa uchaguzi na unaofuata. Magu hajui hili kwasababu halijatokea Tanzania lakini nawaambia leo bila tume huru mwaka kesho mzima utakuwa malalamiko ya kisiasa tu hakuna hoja ya treni au ndege watu watajali. Pamoja na upinzani kuonekana hauna nguvu kuna si chini ya 40% ya watu walipigia kura upinzani na zaidi ya nusu kwenye majiji makubwa. Majiji karibu yote yana Watanzania ambao wanapenda vyama vingi. Kitakachotokea mwaka kesho uchaguzi utakuwa wa kinafiki kama vyama vikubwa vikijitoa.