Kinachohitajikiwa ni Haki, Kinachoitwa Maridhiano ni Upuuzi Unaotakiwa Kupuuzwa

Kinachohitajikiwa ni Haki, Kinachoitwa Maridhiano ni Upuuzi Unaotakiwa Kupuuzwa

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
KUna jambo la kushangaza sana, wauaji na wadhulumaji haki, baada ya kuua watu kwa maelfu, kutrka watu, kuendelea kubambikia watu keshi, baada ya kudhulumu haki, eti wanasema wataanzisha maridhiano. Tuwakatalie hawa watu wapuuzi na upuuzi wao.

Watanzania hawahitaji maridhiano, bali wanahitaji haki. Yakifanyika yafuatayo, nchi itatulia na watu watarejeshewa amani iliyoharibiwa na watawala na CCM:
1. Mwenyekiti na Mkurugenzi wa INEC wakamatwe na kushtakiwa, kwa kutumiwa na wahuni kupindua mamlaka ya wananchi.

2. Tume ya kimataifa pamoja na wachunguzi wa ICC wafanye uchunguzi, watakaobainika kuua wananchi, pamoja na waliowatuma wakamatwe na kushtakiwa

3. Kilichoitwa uchaguzi, haukuwa uchaguzi bali ni uhuni. AU na SADC, wote wamesema hicho kilichoitwa uchaguzi ni NULL AND VOID.

4. Iundwe Serikali ya mpito kwaajili ya kuendesha nchi wakati wa kipindi cha mpito.

5. Ipangwe tarehe ya uchaguzi utakaosimamiwa na ama AU, SADC au UN.

6. Baada ya uchaguzi, ufuate mchakato wa kupata katiba mpya, itakayozingatia haki za watu, itatoa mwongozo wa Tume huru ya uchaguzi, itafuta zile sheria zote za kishetani, kama zile za kudai kuwa eti Rais, makamu wake, Waziri mkuu, Jaji Mkuu na Spika, hawawezi kushtakiwa. Na itamkwe wazi kuwa sheria ile inayokiukwa kifungu cha watu wote kuwa sawa mbele ya sheria, ni NULL and VOID, hivyo wahusika wote kama walitenda makosa washtakiwe ja kuhukumiwa.

Yakifanyika haya, hakuhiajiki hizo hadithi za Maridhiano bandia.
 
Swali lako ni zito sana — linagusa maumivu, msamaha, na utu.
Kukubaliana au kuridhiana na mtu aliyekufanyia ubaya mkubwa (hasa kama alijaribu kukuua au aliua familia yako) si jambo rahisi wala la moja kwa moja.

Lakini hebu tuangalie pande zote mbili:

🔹 Sababu za kutoridhiana (kutokumsamehe)

Mtu huyo aliua au kuumiza watu wasiokuwa na hatia, hivyo ni haki kutaka haki itendeke kwanza.

Msamaha wa haraka unaweza kuonekana kama kupuuza maumivu au mateso ya walioteseka.

Wengine huhisi kuwa kuridhiana ni kusaliti kumbukumbu ya waliopotea.


🔹 Sababu za kuridhiana (kusamehe)

Msamaha unaweza kuwa njia ya kupata amani ya ndani — si kwa ajili yake, bali kwa ajili yako mwenyewe.

Unaweza kuachilia hasira na chuki ambazo zinaweza kukutesa maisha yako yote.

Ikiwa huyo mtu amejuta kwa dhati, anaweza kubadilika na kusaidia wengine wasipitie makosa kama yake.

Dini nyingi (kama Ukristo na Uislamu) zinasisitiza kuwa msamaha ni nguvu, si udhaifu.


🔹 Ukweli wa kati

Unaweza kusamehe bila kuridhiana kabisa.
Maana yake: unaweza kuachilia chuki moyoni, lakini usiwe karibu naye au kumruhusu tena kwenye maisha yako.
Msamaha hauondoi haki — mtu huyo bado anaweza kuwajibishwa kisheria.


---

Kwa hiyo, jibu sahihi linategemea:

Je, unaona toba yake ni ya kweli?

Je, uko tayari moyoni kuachilia?

Je, unahitaji haki kwanza kabla ya maridhiano?


Ungependa nikuandikie mfano wa jinsi mtu angeweza kujibu ombi la maridhiano katika hali kama hiyo — kwa hekima lakini akibaki imara?
 
Neno maridhiano linanipa shida sana wakati kuna watu bado wanakamatwa
 
Maridhiano ni kiinacho kingine cha kuwapumbaza raia wengi wanaotaka utawala wa sheria na haki.
 
Back
Top Bottom