SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Simba imefanya usajili mzuri sana msimu huu na imepambana sana katika mashindano yote ambayo imeshiriki mpaka sasa.
Mechi zote ambazo Simba imepoteza msimu huu au kutoka sare ni kwa sababu ya makosa ambayo chanzo chake kikuu ni kupoteza focus au umakini. Hii inaonyesha timu ni imara sana ila inahitaji kuliangalia hilo maana kila siku linaigharimu timu.
Mechi na Yanga, kupoteza focus kuliifanya ipoteze mechi ambayo ingeweza kabisa kuisha sare. Mechi na Coastal, Fountain Gate, kule CAF mechi ya kwanza dhidi ya Costantine wote mnajua nini kilitokea katika mechi hizi, kupoteza umakini.
Nitagusia matukio matatu ya nje ya uwanja yaliyotokea hivi karibuni ambayo kwa mtazamo wangu nilijua tu yanaenda kuigharimu Simba kwa njia moja ama nyingine. Matukio yote haya naweza kuyaingiza katika tatizo kuu la kupoteza umakini wa nini timu inahitaji na uzito wa jambo lililo mbele.
Soma Pia: FT | Simba SC 2-2 Azam FC | NBC Premier League | Benjamin Mkapa | 24 Februari, 2025
1. Kauli ya Ahmed Ally kuwaita Azam inzi wa chooni. Kwa nini umpe mpinzani hasira ya kupambana dhidi yako? Hii kauli ilinishangaza sana kutolewa kipindi hiki. Focus!
2. Video ya wachezaji wa Simba wakiongozwa na captain Zimbwe kuingia mazoezini jana huku wanacheza muziki. Hakukuwa na umuhimu wa kufanya kitendo hadharani kipindi hiki. Kufanya kitendo kile kuelekea mechi ngumu kama ya leo kinaleta picha ya kwamba wachezaji wameridhika, kwamba wamemaliza na inaonyesha dharau kwa mpinzani wako. Hiki ni kipindi cha kukaa kimya na kumkimbiza mwizi kimya kimya. Focus!
3. Kitendo cha kuruhusu wachezaji waende kwenye harusi ya Aziz Ki. Nilimuona Chamou kwenye harusi ya Aziz Ki, sina uhakika wachezaji gani wengine walikuwepo. Ni jambo la kushangaza kuona Chamou alikosa mechi ya Namungo kisa harusi ya Aziz Ki. Ile mechi, Che Malone angeumia kama alivyoumia leo, Simba haikuwa na mbadala wake kwenye benchi. Hili jambo lilinifikirisha sana, nikajiuliza maswali mengi. Yaani mpinzani wako kaamua kufanya upuuzi katikati ya msimu na wewe unajiunga katika upuuzi wake? Nafikiri kuna hali ya kutotambua uzito wa upinzani wa Yanga wa ndani na nje ya uwanja katika mapambano haya ya ubingwa.
Pamoja na kwamba msimu huu Simba inajenga timu ila ikikosa ubingwa ijilaumu tu yenyewe. Yanga hapo kati walivurugana sana. Ilihitaji tu kukeep focus ndani na nje ya uwanja baasi.
Nafasi ya Simba kuchukua ubingwa bado ipo ingawa kwa makosa haya imekuwa ngumu zaidi. Kilichobaki ni kuhakikisha inashinda mechi zote zilizobaki ikiwemo derby.