Kinachojiri bungeni leo Ijumaa tarehe 14 Machi 2014

Kinachojiri bungeni leo Ijumaa tarehe 14 Machi 2014

Skype

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
7,266
Reaction score
1,633
Karibuni ndugu wajumbe wa jf, sina mengi isipokuwa nawapeleka moja kwa moja mjini dodoma kufuatilia shughuli za bunge.

Kwako Chabruma na wadau wengine mlioko dodoma
 
Last edited by a moderator:
Sitta kamaliza kuapa sasa anasaini kiapo
 
Sasa ni zamu ya Samia Suluhu kuapa
 
Tunashukuru kwa kutupa taarifa,endelea kutujuza mkuu
 
Mzee Kificho anatoa hotuba ya kuaga kiti na wajumbe
 
Kificho anamsifu Sitta na kuamini kua ataliongoza bunge kwa mujibu wa falsafa yake ya kasi na viwango, pia anampongeza Samia na anaamini watashirikiana na Sitta.
 
Kificho anawasifia wajumbe kwa kuchagua viongozi based on gender, anawapongeza Sitta mzee wa kasi na viwango na Samia
 
Kificho anaendelea kuwapongeza pia wajumbe pamoja na katibu wa bunge kwa kumchagua kuwa mwenyekiti wa muda
 
Kificho anasema kua kazi ilikua ngumu kuwaongoza watu mchanganyiko hii ni pamoja na utofauti wa makundi yaliyokuwemo
 
Kificho anaendelea kusema ili kupata katiba bora ni lazima kutanguliza maslahi ya taifa, pia anawasihi wajumbe kushikamana kwa kutoa hoja zenye mashiko pia kukubaliana kutanzua matatizo pale wanapotatizika
 
Kificho anamalizia kwa kuwashukuru wajumbe wote hususani wajumbe wa kamati ya kanuni pamoja na kamati ya maridhiano
 
Kificho kasema mengi na anawashukuru wadau wote waliompa ushirikiano tangu mwanzo hadi leo, na sasa anamkaribisha mwenyekiti wa kudumu ndugu Sitta kwenye kiti chake.
 
Pandu anaschia kiti kwa uchungu anasema ni kitamu
 
Back
Top Bottom