Kinachojiri bungeni leo Ijumaa tarehe 14 Machi 2014

Kinachojiri bungeni leo Ijumaa tarehe 14 Machi 2014

Mwenyekiti wa kudumu Sitta sasa anazungumza
 
Karibuni ndugu wajumbe wa jf, sina mengi isipokuwa nawapeleka moja kwa moja mjini dodoma kufuatilia shughuli za bunge.

Kwako Chabruma na wadau wengine mlioko dodoma

pamoja' mkuu "Skype"
...nasikia hicho kiti cha M/kiti ni KITAMU!
 
Last edited by a moderator:
tupeni update za kutosha arusha hakuna umeme
 
Sitta anasema zitatumika siku 3 kuwaapisha wajumbe, na kwa kuzingatia kua jumatatu ni siku ya kuanza shughuli za kujadili rasimu.
Sasa anamwita Werema ili atoe hoja ya kutengua kanuni ili leo wajumbe waanze kuapishwa hadi saa 3 za usiku.
 
Kwa mujibu wa Sitta ni kwamba Jumatano rais atakuja kuzindua bunge kama nimemuelewa
 
Sitta anasema jumatatu warioba atawasilisha rasimu jumanne na tano ni raisi jk atahutibia na kama kunamabadiliko atatangaza
 
Pia wajumbe wataendelea kuapishwa toka leo hadi Jumapili
 
...kuanzia leo bunge maalum litakuwa linaendelea hadi saa3 usiku! Kasema Mh. Sitta.
"leo, kesho na J'pili kuanzia saa5 asubuhi hadi saa3 usiku!
 
Sitta anawatahadharisha kua kwa sasa atasimamia kanuni na hatapenda kulaumiwa kwa kutekeleza wajibu hasa kwa wale wajumbe waliozowea kufanya vituko kama kupiga kelele, kusemasema ovyo bila utaratibu.
 
Sitta anamwita sasa mwanasheria mkuu wa serikali ili atoe hoja ya kuwezesha bunge kukutana hadi saa 3 usiku
 
...kuanzia J'tatu kwa muda wa siku3, wajumbe watakuwa wanajadili, kabla ya kuanza kazi ya Kamati mbalimbali.
 
Jaji Werema anatengua kanuni ili bunge liendelee hadi saa3 usiku!
 
Werema anaomba kanuni ya 14 fasili ya 5 ili bunge liweze kukaa hadi saa 3 usiku
 
Werema kamaliza kutoa hoja ya kutengua kanuni ya 14
 
...kauli inatenguliwa kwa ajili ya kesho na J'pili.
"sasa KASI IMEANZA"
NDIYOOOO

WALIO SEMA NDIYO WAMESHINDA.
 
Hoja imeungwa mkono na imepita na kinachofuata ni uapishwaji wa wajumbe kuanzia muda huu hadi saa 3 usiku na uapishwaji utaendelea tena kesho na kesho kutwa.
 
Kwa kifupi hayo ndiyo yaliyojiri bungeni jioni hii na sina la ziada isipokua namshukuru msimamizi wa jukwaa hili, pia mafundi mitambo wote wa jf, bila kuwasahau wajumbe wote walionipa ushirikiano.

Hadi wakati mwingine, mimi ni Skype nasema kwa heri kwa sasa.
 
Kuna kitu wadau sijaelewa Jk anazindua Bunge na kuondoka zake au atazindua pamoja na kuhutubia? Hapa sijaelewa mambo yanaedaje.
 
Back
Top Bottom