Kificho anamsifu Sitta na kuamini kua ataliongoza bunge kwa mujibu wa falsafa yake ya kasi na viwango, pia anampongeza Samia na anaamini watashirikiana na Sitta.
Kificho anaendelea kusema ili kupata katiba bora ni lazima kutanguliza maslahi ya taifa, pia anawasihi wajumbe kushikamana kwa kutoa hoja zenye mashiko pia kukubaliana kutanzua matatizo pale wanapotatizika
Kificho kasema mengi na anawashukuru wadau wote waliompa ushirikiano tangu mwanzo hadi leo, na sasa anamkaribisha mwenyekiti wa kudumu ndugu Sitta kwenye kiti chake.