Sitta anasema zitatumika siku 3 kuwaapisha wajumbe, na kwa kuzingatia kua jumatatu ni siku ya kuanza shughuli za kujadili rasimu.
Sasa anamwita Werema ili atoe hoja ya kutengua kanuni ili leo wajumbe waanze kuapishwa hadi saa 3 za usiku.
Sitta anawatahadharisha kua kwa sasa atasimamia kanuni na hatapenda kulaumiwa kwa kutekeleza wajibu hasa kwa wale wajumbe waliozowea kufanya vituko kama kupiga kelele, kusemasema ovyo bila utaratibu.
Hoja imeungwa mkono na imepita na kinachofuata ni uapishwaji wa wajumbe kuanzia muda huu hadi saa 3 usiku na uapishwaji utaendelea tena kesho na kesho kutwa.
Kwa kifupi hayo ndiyo yaliyojiri bungeni jioni hii na sina la ziada isipokua namshukuru msimamizi wa jukwaa hili, pia mafundi mitambo wote wa jf, bila kuwasahau wajumbe wote walionipa ushirikiano.
Hadi wakati mwingine, mimi ni Skype nasema kwa heri kwa sasa.