Kinachokukera ni nini? Pilipili ipo shamba unawashwa na nini? Tuseme NI wivu au Roho mbaya Tu!

Kinachokukera ni nini? Pilipili ipo shamba unawashwa na nini? Tuseme NI wivu au Roho mbaya Tu!

Tsyamatsy

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2023
Posts
265
Reaction score
421
Ni kitu cha kipumbavu Sana na cha kijinga na Roho mbaya Kwa baadhi ya watu kukejeli wanawake wenye watoto kuolewa.

Hiki kimejitokeza Sana wiki hii kufuatia Hamisa Mobeto kutolewa mahali na Aziz Ki.

Kumekuwa na maneno mengi ya kuwakejeli huyo bint na huyo kijana, kisa eti dada kazaa ana watoto wa wanaume wengine, wengine wamekuwa watabiri eti Ndoa hiyo haitadumu!

Wote wenye mtizamo hasi nawaambia kuwa HERI ya huyo aliyezaa na watoto wake wanajulikana kuwa NI wafulani.

Sidhani Kama kuna mtu anapenda matatizo hapa duniani, lakini inatokea Tu.

Binadamu ili azaliwe, NI kitendo cha kujamiiana mwanamke na mwanamme, na katika tendo Hilo Muumba aliamua mwanamke ndie abebe mimba. Lakini baadae kunakuwa na mahusiano hafifu yanayosababisha kutengana au kutokuoana baada ya kuzaa Mtoto.

Iweje kuwakebehi hao wanawake mbona hatushikilii mabango Kwa wanaume ambao tunawajua fika wamezaa na Wana watoto, mfano hao waliozaa na huyo Hamisa, mbona hamuwasemi kuwa hawafai kuona sababu Wana watoto tayari!

Kila mtu ana bahati yake uwezi kuizuia na Tusiwanyanyapae Akina mama sababu ya jinsia zao.
 
Sidhani Kama kuna mtu anapenda matatizo hapa duniani, lakini inatokea Tu.
Inatokea kwa kutaka wenyewe na uzembe au tamaa.
Condom, vidonge, shindano na vijiti vya kuzuia mimba vipo.
Njia ya za asili kama kuchomoa nje, mzunguko wa hedhi na kujizuia kabisa vipo.
 
Mimi sina tatizo.na single mazas kuolewa. Wanaolewa sana na ni jambo zuri. Hongera zake Hamisa kwa kuolewa...sina wivu lakini wataachana tu.
Tusihukumu Leo! Hayo NI majaliwa ya Muumba! Wakati mwingine unaona NI kunguru kumbe NI njiwa
 
Your boyfriend is waiting for other niggas to finish talking about their careers and businesses so he can talk about Aziz Ki & Hamisa Mobetto.



476833379_2625230401003404_5573767746912223267_n.jpg


Katika kukumbushana tu.
 
Wanawake wasibebe mimba hovyo hovyo. Kuolewa si bahati ni jukumu la kijamii la mwanamke.
Mnapokuwa katika mahusiano siku za mwanzo mnapeana ahadi chungu Tele, na hapo ndipo chanzo cha mimba, baada ya kuzoeana ndipo mnapoanza kufahamiana tabia na ndipo tabia za hasi na chanya kutokaa pamoja. Hatimae mnaachana na mwanamke ameshazaa, ndipo chanzo cha single mum! Tusiwanyanyapae, Labda sio chanzo NI yeye Labda NI mwanaume ndio chanzo, tusiwahukumu wote, tuwe ' fair ' pande zote
 
Mademu wapunguze mapicha picha,yaan hamisa hata anaetoka nae siku moja lazima apige nae mapicha picha
 
Back
Top Bottom