Kinachokukera ni nini? Pilipili ipo shamba unawashwa na nini? Tuseme NI wivu au Roho mbaya Tu!

Kinachokukera ni nini? Pilipili ipo shamba unawashwa na nini? Tuseme NI wivu au Roho mbaya Tu!

Mkuu mwanamke kuishi na mwanaume wazazi hawana taarifa ni umalaya. Ikitokea mimba mkaachana ni matokeo ya umalaya.
Kama mmependana kwanini msipelekane kwa wazazi?
Mkuu fafanua hapo, NI mwanamke Tu NI Malaya au hii pia mwanaume naye NI Malaya? Yaani wote?
 
Ni kweli niko 34
Sawa mkuu, wewe Kama mwanangu, Sisi Tumeyaona, haya NI maisha kadri unavyoishi utajifunza mengi, na Mungu akikujalia kufika above 55 utakuwa mzoefu WA maisha.
Maisha ya ujana haswa uswahilini mijini, maisha vijana kukalishana unyumba NI suala lililozoeleka na ndipo Ndoa zingine zinapoanzia na watu wakaishi mke na mume Hadi kifo. Lakini kuna wengine NI Leo kakaa na huyu na kesho kakaa na Yule, hii NI Kwa mwanamke na mwanaume, Kwa iyo Kama NI Malaya basi NI wote sio kubagua msichana pekee kwani neno Malaya ili likamilike lazima kuwa na jinsia zote mbili. Kwa iyo nakushauri Fanya tafiti, Sisi tulioishi uswahilini sio kitu kigeni, tafiti maisha ya uswahilini baadae njoo na ushahidi.
 
Mimi sina tatizo.na single mazas kuolewa. Wanaolewa sana na ni jambo zuri. Hongera zake Hamisa kwa kuolewa...sina wivu lakini wataachana tu.
ndo maana DRC inagombaniwa,wasiojua wanailaumu DRC wenye akili tunawalaumu wanaoigombania,
 
Hao walio olewa na kuachika tofauti na Hamisa.
Sitaki kuwahukumu wote nataka kupinga kumtetea Hamisa.
Huyo alijua kabisa Diamond yupo na mtu akakubali kushiriki naye ngono bila kuzuia mimba.
Kama alikosea kwa Majizzo kwanini alirudia kosa kwa Diamond?
Mhh! Hapa mimi sina la kusema!
Samahani Mimi lengo la Uzi huu si kumtetea Hamisa Bali ni Kwa Akina mama wenye watoto bila ya wanaume, ila Hamisa amekuwa mhusika kipindi Hiki.
 
Mkuu fafanua hapo, NI mwanamke Tu NI Malaya au hii pia mwanaume naye NI Malaya? Yaani wote?
Mkuu, Jamii yetu imeamua kumuelewa mwanaume malaya na kumsamehe kwa umalaya wake ila si mwanamke.
 
Ni kitu cha kipumbavu Sana na cha kijinga na Roho mbaya Kwa baadhi ya watu kukejeli wanawake wenye watoto kuolewa.

Hiki kimejitokeza Sana wiki hii kufuatia Hamisa Mobeto kutolewa mahali na Aziz Ki.

Kumekuwa na maneno mengi ya kuwakejeli huyo bint na huyo kijana, kisa eti dada kazaa ana watoto wa wanaume wengine, wengine wamekuwa watabiri eti Ndoa hiyo haitadumu!

Wote wenye mtizamo hasi nawaambia kuwa HERI ya huyo aliyezaa na watoto wake wanajulikana kuwa NI wafulani.

Sidhani Kama kuna mtu anapenda matatizo hapa duniani, lakini inatokea Tu.

Binadamu ili azaliwe, NI kitendo cha kujamiiana mwanamke na mwanamme, na katika tendo Hilo Muumba aliamua mwanamke ndie abebe mimba. Lakini baadae kunakuwa na mahusiano hafifu yanayosababisha kutengana au kutokuoana baada ya kuzaa Mtoto.

Iweje kuwakebehi hao wanawake mbona hatushikilii mabango Kwa wanaume ambao tunawajua fika wamezaa na Wana watoto, mfano hao waliozaa na huyo Hamisa, mbona hamuwasemi kuwa hawafai kuona sababu Wana watoto tayari!

Kila mtu ana bahati yake uwezi kuizuia na Tusiwanyanyapae Akina mama sababu ya jinsia zao.
Kabla sijatoa maoni yangu naomba kujua wewe Ke au Me.
 
Mimi sina tatizo.na single mazas kuolewa. Wanaolewa sana na ni jambo zuri. Hongera zake Hamisa kwa kuolewa...sina wivu lakini wataachana tu.
Kwa ninj wataachan na hawatazeeka pamoja?
 
Back
Top Bottom