Kinachomgharimu Mugalu ni kuwa eneo sahihi muda wote

Kinachomgharimu Mugalu ni kuwa eneo sahihi muda wote

Cvez

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2018
Posts
4,405
Reaction score
13,411
Kama shabiki wa Simba kindakindaki nimekaa nikiiangalia timu yangu hasa eneo la ushambuliaji. Ambako kuna Bocco, Kagere na Mugalu. Katika huyu Mugalu sasa anaweza kupata nafasi 5 za kufunga ila akafunga goli moja tu. Tukirudi kwa Kagere yeye akipata nafasi ya kufunga katika mbili atatupia at least moja.

Na kumekua na mjadala kwa nini kocha Gomez anapenda kumtumia Mugalu zaidi badala ya Kagere ambae yupo vizuri zaidi kwenye umaliziaji. Ila katika uchunguzi wangu mfupi Mugalu ni mhanga wa uchezaji wake, anakosa magoli mengi kutokana na jinsi anavyojiposition vizuri katika eneo la ushambuliaji hii inasababisha hata ule mpira ambao haukua na hatari Mugalu ataunasa na kufanya attempt. Ukirudi kwa Kagere akipata mpira eneo ambalo halina madhara na yeye pia hana madhara yoyote.

Katika nafasi 5 za Mugalu 3 au 4 amehusika moja kwa moja kuzitengeneza au amekaa katika position ambayo ilimpa uwezo wa yeye kuunasa mpira na kufanya attempts nyingi. Kuna muda namuelewa Gomez kwa nini anamuanzisha Mugalu badala ya Kagere anampa vitu vingi zaidi katika eneo la ushambuliaji. Ingawa kama shabiki kuna muda Mugalu ananikera kwa nafasi anazozipoteza ila ukitaka kujua uzuri wa Mugalu muangalie Kagere yeye hua anapata nafasi chache tu za kufunga na ni kwa sababu hana uwezo wa kujitengenezea nafasi kama Mugalu. Mpira ukifika kwa Kagere mara nyingi upo tayari kwa kupasia golini.

Muhimu ni Mugalu afanye mazoezi ya ziada katika finishing.
 
Mugalu ni striker mzuri Sana, Meddie uwezo umepungua ila Bocco bado wa Moto.

Kutumia strikers wawili ni muhimu Sana hasa kwa local matches ili kuendelea kulinda viwango vyao.

Simba tunahitaji striker damu changa kama Prince Dube wa kuongeza ufanisi
 
Katika mastriker wa Simba hakuna anayemfikia John Bocco katika kutengeneza nafasi.

Kagere conversion rate yake ni kubwa kwa sababu anaweza kutumia miguu yote bila shida lakini anafanya maamuzi kwa haraka zaidi kuliko wengine.
 
Back
Top Bottom