Kinachosababisha watu wengi kuharibu maisha ya watu makazini ni wivu, uchawi na kufuatilia maisha ya mtu ambayo hayana mahusiano na kazi mnayofanya

Kinachosababisha watu wengi kuharibu maisha ya watu makazini ni wivu, uchawi na kufuatilia maisha ya mtu ambayo hayana mahusiano na kazi mnayofanya

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Utasikia huyu jamaa anakunywa kila siku. Wewe inakuhusu nini?

Utasikia jamaa huwa haishiwi hata katikati ya mwezi. Shida yako nini?

Utasikia jamaa mtaani anamdemu kibao. Tatizo nini?

Dili na masuala yanayokuunganisha na mtu kwenye kazi sio maisha yake binafsi kiasi cha kumuonea wivu na kumroga.
 
Unapokuwa mbele ya coworker /workmate try to live like a commoner and play low KEY.

Katika kazi unabidi usjinge mazoea na WATU na sio kazini hata kwenye FAMILIA yako na mtaani ishi Kama stranger.

Hakikisha hawakujui una nini unamiliki nini au una mafanikio kiasi gani.
 
Umesahau kitendo cha kutembea (kudate) na mfanyakazi mwenzio hii ni hatari sana kwa mustakabali wa maisha yako kwa ujumla.

Ila tunajifanyaga Kama hatuelewi

Matatizo yanaanzia hapo
 
Unapokuwa mbele ya coworker /workmate try to live like a commoner and play low KEY.

Katika kazi unabidi usjinge mazoea na WATU na sio kazini hata kwenye FAMILIA yako na mtaani ishi Kama stranger.

Hakikisha hawakujui una nini unamiliki nini au una mafanikio kiasi gani.
Vipi kama mtu alishakosea watu wakamjua je anaweza kuanza upya maisha
 
Vipi kama mtu alishakosea watu wakamjua je anaweza kuanza upya maisha
Yes inawezekana ila wakati unaanza upya iwe siri yako.

Ukiishi Kama stranger watu hawawezi kukudhuru iwe katika. familia yako ,kazini hadi mtaani .na Heshima itakuwa kubwa sana.

Kisaikoloji MTU kitu ambacho hana uhakika wa kukipata huwa anakithamini sana.

So watu wakiona unakuwa haupatikani katika zone zao Ila unapambania dreams zako utakuwa valuable sana haijalishi una pesa au hauna.
 
Back
Top Bottom