Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
"Sir Alex Ferguson kwenye Kanuni zake 9 kuhusu Nidhamu naomba nimnukuu kanuni namba 4, "Never ever, cede control" usikubali kupoteza Mamlaka yako mbele ya wachezaji"
"Kupitia hii Roy Keane alipokosoa wenzake mbele ya Media basi Fergie alivunja mkataba wake, Van Nisterloy na kipaji chake alipokosoa mamlaka akauzwa Real Madrid, hii ina maana hakuna mkubwa kuliko timu"
"Kinachotokea kwa Mkude ni kuishi kimazoea, yakajenga tabia, tabia ni kovu halifutiki kwa sabuni, Simba haipo kule alipozoea, wameset standards, asipobadilika atapata wakati mgumu sana, abadilike"
"Bila mkazo kwenye nidhamu, ipo siku Wachezaji watakupangia muda wa mazoezi, watakupangia aina ya mazoezi na watakupangia kikosi, lazima Sheria zifuatwe, hakuna mkubwa kuliko Taasisi"
Maneno ya Farhan Kihamu @jr_farhanjr kwenye SPORTS ROUND UP ya @cloudsfmtz