Kinachotushinda Wabantu kuchora na kupanga miji ni nini?

Tuachane na suala la mpango mji, nyanja ipi ya kimaendeleo ambayo tunaimudu kwa ufanisi?

Kama kila sehemu ni utumbo tu kwanini tutarajie hapo kwenye mipango miji kutakua na afadhari?

Jibu la swali lako ni rushwa na nafasi kushikiliwa na watendaji wasiokua na uwezo
 
Swali. Wewe kama baba/mama mwenye nyumba, watoto wako watajipangia ramani ya Kiwanja cha familia yako hovyo hovyo, ukawachekea na kuwaacha tu ?
 
Ajabu ni kwamba Maafisa mipango miji wapo humuhumu na pengine wamechangi HII MADA
 
Sio kuchora na kupanga tu, bali hata kuheshimu kile tulichokipanga na kukichora tunashindwa

Wee angalia Sinza zilivyomegwa open space na uchafu wa misururu ya vibanda unavyoendekezwa

One of the former PM akiwa bado kazini unakuta nyumbani kwake ana mabanda ya ng'ombe ktk eneo ambalo ni makazi ya Viongozi wa juu

Ukiangalia background yake yeye na ng'ombe walikuwa kama part and parcel of the family

Kwa hiyo kuna vitu mpaka vitoke kwenye mabongo yetu itachukua Karne kadhaa
 
Tunamudu kuwadhibiti Chadema na kutukuza viongozi...
 
Uko sahihi kabisa, ule mpango wa MKURABITA haukuwa suluhisho
 
Yani hata Gaza wametushinda. Aibu
 
Rushwa tumuachie nani shida ndio hiyo
 
Alafu unasikia nyumba Iko karibu na barabara
 
Ajabu ni kwamba Maafisa mipango miji wapo humuhumu na pengine wamechangi HII MADA
Inawezekana kweli wapo, lakini hata wakipeleka mapendekezo ya kitaalam, wafanya maamuzi wana vipaumbele vyao. Inabidi uangalie chanzo halisi cha tatizo vinginevyo utalaumu watu bure.
 
Duh! Mkuu hata miji mipya wanashindwa, mana kweli tumekosea toka awali lakini vipi maeneo yasiyokaliwa, kwanini mipango isifanyike mapema?
 
= kibali.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Siasa ndo inaharibu mambo...
Enzi hizo jiji la Mwanza lilikuwa na mradi wa sustainable cities program, mjamaa mmoja akapel3kwa nje kusomea mipango miji degree ya uzamili... aliporejea tu alikaa miezi michache tu akateuliwa kuwa DED...
 
Hata Syria iliyotoka vitani bado kuna mipango mizuri na michoro mizuri kuliko sisi tusiokua na vurugu.
kwa kweli sisi akili zetu ni za kuvukia barabara. Pale kokobeach parking mwaka wa 3 huu city inachukua mapato kuweka sakafu hawataki ni matope matupu. na bado hawaweki taa fukwe nzima giza wakati investiment zake ni kubwa sana.

watanzania hawa weledi, watanzania hawawezi fikiri kwa manufaa yao na vizazi vyao. namalizia watanzania ni washamba wa maendeleo
 
Ardhi Sio kipaumbele cha Serikali, Huwezi kupanga Ardhi ambayo siyo ya kwako. Tanzania tuna sheria ya Utwaaji Ardhi, Kabla ya kuchora Hayo maua unayo yaona na hivyo vibox, inatakiwa ulipe kwanza Fidia.

Nani analipa hiyo fidia? Serikali Ardhi sio kipaumbele chake, hivyo fidia atalipa pale ambapo kuna Kipaumbele chake. Huko kwingine acha kujiendee. Ndio maana Si Ajabu kukuta Kijiji kiko ndani ya Hifadhi, Eneo la Uwanja wa ndege limevamiwa, n.k

Miji yetu itaweza kupangika vyema kama Serikali italipa Kipaumbele suala la Ardhi kwa maana ya;
1. Upangaji
2. Upimaji
3. Kusimamia Uendelezaji. Tofauti na Hapo tutakua na Makazi Holela (Squatter) nchi nzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…