Kuvuka barabara tu ndio tunaweza 😄😄kwa kweli sisi akili zetu ni za kuvukia barabara. Pale kokobeach parking mwaka wa 3 huu city inachukua mapato kuweka sakafu hawataki ni matope matupu. na bado hawaweki taa fukwe nzima giza wakati investiment zake ni kubwa sana.
watanzania hawa weledi, watanzania hawawezi fikiri kwa manufaa yao na vizazi vyao. namalizia watanzania ni washamba wa maendeleo
Mkuu sa kazi ya maafisa ardhi ni nini? Malengo ya Wizara ni kutatua migogoro tu bas lakini uchoraji na upimaji mtajua wenyewe au siyo?Ardhi Sio kipaumbele cha Serikali, Huwezi kupanga Ardhi ambayo siyo ya kwako. Tanzania tuna sheria ya Utwaaji Ardhi, Kabla ya kuchora Hayo maua unayo yaona na hivyo vibox, inatakiwa ulipe kwanza Fidia.
Nani analipa hiyo fidia? Serikali Ardhi sio kipaumbele chake, hivyo fidia atalipa pale ambapo kuna Kipaumbele chake. Huko kwingine acha kujiendee. Ndio maana Si Ajabu kukuta Kijiji kiko ndani ya Hifadhi, Eneo la Uwanja wa ndege limevamiwa, n.k
Miji yetu itaweza kupangika vyema kama Serikali italipa Kipaumbele suala la Ardhi kwa maana ya;
1. Upangaji
2. Upimaji
3. Kusimamia Uendelezaji. Tofauti na Hapo tutakua na Makazi Holela (Squatter) nchi nzima.
Afu dunia ya sasa mitaro inakula sana nafasi ya barabara, kwa miaka hii 2000 mitaro ilitakiwa ipite chini kwa chini tu. Kwanza unaepusha mengiNa mimi nachomekea ,sio mtaalamu wa ujenzi( najitetea mapema kabisa).Hivi wanapotengeneza mamitaro mjini halafu hawayafuniki huwa wana maana gani hawa watu?! Sielewi aisee.
Siku kondoo wakijuwa kutumia vyoo, kila kitu watakiweza.
Unauliza swali kubwa namna hilo kwa kondoo ambao mpaka leo hawajuwi namna ya kutumia choo?
tafadhali watendee haki.
Nina jirani zangu washenzi wameuziana maeneo kienyeji mpaka wamezibiana na kukosa njia sasa wanakuja kwangu kulazimisha njia wakati eneo langu nimelipima na lina hati.. Nilichofanya nimewafungia kila kona watajuana na waliowauzia huko
Mkuu angalia South Africa ilivyo, matunda ya Wazungu. Kwa Tanganyika Nyerere alifeli hapo tu, kuwaondoa kabla hatujajiwezaTulikosea sana kuwaondoa wakoloni weupe.wangekuwepo Hadi Sasa miji yetu Ingekuwa imepangika vizuri na kuvutia .Mfano ukiangalia masaki,mikocheni,upanga,posta kote huko walipanga wakoloni lakini linganisha na mwananyamala,buguruni,tandika,mbagala ambako walipanga waafrika.