Na bado hamjasema mafisadi nyie wa CCM. Wanafiki wakubwa. CHADEMA imetangaza maandamano halafu wewe chawa unaleta stori za kijinga.
Naomba nikuelimishe wewe chawa wa mama Samiah na CCM kwamba;
1. CCM ndio yenye madaraka. Hivyo peleka hasira zako kwa CCM kwanini haiwajali wanyonge, achana na CHADEMA ambayo haina madaraka. Yani unamuacha mwenye mamlaka ya kuhudumia wanyonge, halafu unaleta lawama za kijinga kwa CHADEMA ambayo ni outsider.
2. CCM ndio imejaza wabunge wengi bungeni asilimia 98%, peleka hasira zako za kinafiki kwa wabunge wa CCM kwanini hawajali wanyonge?. Unalalamika CHADEMA ambayo Ina mbunge moja wakuchaguliwa Tena na chama hakimtambui unaacha wabunge wote wa CCM waendelee na ujinga wa kuongeza tozo kwa Wananchi.
3. CCM imejaza madiwani asilimia 98% nchi nzima na kushikilia Halmashauri zote nchini, nenda kapeleke hasira zako za kinafiki CCM. Unailaumu CHADEMA kwa kutokujali wanyonge wakati CCM inayopiga mapesa ya Halmashauri unaichekelea na kuilamba makalio, very stupid.
4. CCM ndio inashikilia Mitaa na Vijiji karibia vyote Tanzania, na ni asilimia 97%, ila wewe kwa unafiki wako unailaumu CHADEMA kwa kutokujali wanyonge wakati hiyo CCM ndio imeshikilia uongozi huko Chini kabisa kwa wanyonge.
5. CCM ndio yenye bajeti na sera. Yani CCM ndio inaamua pesa ziende wapi na zifanye Nini. Lakini Cha ajabu wewe Mnafiki unaiacha CCM yenye kupokea Kodi za Wananchi kupitia serikali yake na kuifuja hovyo, ila wewe unailalamikia CHADEMA haipokei Kodi Wala haisimamii sera ya Taifa.
Mwisho, nakushauri punguza ujinga na unafiki. Huyo makonda ni mtoa Habari Kama Ally Kamwe wa Yanga au Ahmed Ally wa Simba Hana mamlaka yeyote ya kutetea wanyonge. Yeye ni chawa wa mama, yupo pale kutoa taarifa za chama. Ndio maana juzi ulimuona anatangaza ratiba ya mkutano wa Samiah Zanzibar.
Peleka malalamiko yako CCM na Kwa huyo makonda na uache kutafuta kiki kupitia CHADEMA. Subiria siku CHADEMA ikichukua nchi halafu ikashindwa kuwajali wanyonge, ndipo ulete povu.