Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
MUHIMU: Mshahara wa Raisi na mawaziri uwekwe hadharani ili tujue tunawalipa sh.ngapi kwa mwezi.
hapa kazi na wakati umeme hamna hiyo kazi itafanyika vp?
Funny enough hata huku Chato Magufuli hakubaliki kama Lowassa
FISADI=LOWASA LOWASA=JIZI NB:Huwezi kula matapishi yako
Hayo ni maandalizi mazuri. Hakuna sababu ya kupoteza muda baada ya uchaguzi. Wananchi wanakiu ya mabadiliko. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Tupo vizuri... Mnajua mambo tuliyoyafanya katika majimbo 208!!! CCM is back again where it belongs!! Thanks Comrade MAGUFULI for making us laughing again!!!
Acha kupotosha watu,Wewe uko chato ya wapi?
LOWASSA anatisha mnatumia jina lake kumnadi mgombea wenu?Dkt. Magufuli amelipa jopo hili majukumu yafuatayo:
1. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itabana matumizi, ikiwemo manunuzi ya umma, posho za vikao na matumizi ya magari, ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;
2. Kuchunguza na kupendekeza maeneo ambayo Serikali itaongeza mapato mara moja bila hatua za kibajeti kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa;
3. Kuchunguza na kupendekeza maboresho makubwa katika mfumo wa utendaji na utumishi na ufanisi katika Serikali;
4. Kupitia kodi na ushuru wenye usumbufu kwa wafanyabiashara wa ngazi zote, wakulima, wafugaji na wavuvi iwapo unaweza kurekebishwa bila kuathiri bajeti ya Serikali inayotekelezwa sasa.
5. Kupitia sheria zote za nchi na kuorodhesha Sheria ambazo zinapaswa kubadilishwa haraka ili kuharakisha mabadiliko ya kweli na ya haraka ambayo ameyaahidi kwa Watanzania;
6. Kupitia na kuorodhesha masuala yote na kero zote zinazosubiri maamuzi ya Serikali ili atoe maamuzi kuanzia siku ya kwanza atakapoapishwa.
7. Kupendekeza miundo na idadi ya Wizara na kutengeneza rasimu za mikataba ya kazi kwa Mawaziri, Makatibu Wakuu na watendaji wengine wakuu atakaowateua mara baada ya kuapishwa.
8. Kupendekeza njia za haraka za kumaliza kero za watumishi wa umma, hasa walimu, askari, madaktari na wauguzi, ili aanze nao kazi wakiwa na ari na morali ya kusukuma mabadiliko ya kweli.
9. Kutengeneza rasimu ya mpango-kazi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi alizozitoa kwenye kampeni, hasa upatikanaji wa ajira kwa haraka na umeme wa uhakika;
10. Kupendekeza muundo wa kitaasisi na utaratibu muafaka wa kutekeleza ahadi ya kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa nchini.
Dkt. Magufuli ameazimia kuanza kazi mara moja kwa bidii kubwa na maarifa mapya.
Imetolewa na:-
January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni