mambo yote uliandika hapo ni poumba tupu.
Halafu ukahangaika sana kuzijibu 'pumba'! Ni nani aliyepungukiwa na akili hapo?
Kwanza elewa kuwa kutoa ushauri kuhusu sera ni tofauti na kulalamika kuwa unachafuliwa binafsi;
Kuingiliwa mawasiliano ambayo ni ya mtu na mtu faragha, sio kuvunjiwa heshima? Tena watu wanaofanyiwa kitendo hicho wakiwa wastaafu, ambao kwa raia wa kawaida angedhani ni watu wanaoheshimika ndani ya chama!
Kama wanayo madudu yao yaliyogundulika ndani ya chama, haya yasingeweza kushughulikiwa kwa taratibu za kichama huko huko ndani ya chama?
Sasa unajitoa ufahamu. Ni sehemu ipi Kinana na Makamba walipolalamikia kuwa "ushauri wao hausikilizwi". Kwa hiyo malalamiko yao hayo ndio iliyokuwa sababu ya wao kudukuliwa mawasiliano yao?
Kwanza elewa kuwa kutoa ushauri kuhusu sera ni tofauti na kulalamika kuwa unachafuliwa binafsi; na kutoa ushauri haina maana lazima ushauri huo ukubaliwe na aliyeko madarakani, ndivyo demokrasi ilivyo. Nyerere alishauri mabenki yasizwe lakini Mkapa akayauza. Nyerere alizuia Azimio la Arusha lisifutwe, lakini Mwinyi akalifuta kule Zanzibar; Nyerere alikuwa akiongelea sera, hakuwa naongelea kuchafuliwa na mtu, na bado viongozi walioko madarakani walipuuza sehemu ya ushauri wake.
Pamoja na yote hayo, Mwalimu Nyerere hakudhalilishwa na hao uliowataja. Hakudukuliwa maongezi yake, na wala hakuitwa kwenye kamati za kipuuzi kuchunguza malalamiko yake.
Huna hata akili ya kutofautisha hali hizi mbili ambazo ziko wazi kabisa?
Mwalimu alikuwa na uhuru na haki ya kusema alichoona hakiko sawa, na heshima yake haikudhalilishwa na Mwinyi, na Mkapa. Huyu unayetetea wewe ana nini cha ziada watu wasitoe maoni yao?
Pili: kama huumizwi na hao jamaa zako, hii ilikuwa topiki kuwahusu wao, imekuvuta nini kuwatetea. Kama unaichukia CCM yoteM, na unajua wao ni sehemu ya CCM usingechukua sides; ungewaacha wafu wazikane wao kwa wao. Unachozungumza hapa ni kuwa CCM yao ilikuwa nzuri kuliko CCM ya leo, halafu bado unasema CCM huitaki; come on.
Hapa pia unaonyesha upungufu wa uwezo wako wa kufikiri.
Kuna pande mbili zinazohusika kwenye mzozo huo.
Kutoshangilia upande ulioko wewe hakuna maana kwamba naunga mkono upande usioupenda wewe.
Anayechukua jukumu la kukiuka taratibu na kujifanya yeye ndiye mwenye haki ya kujua na kuamua kila kitu, tena kwa kujinufaisha yeye mwenyewe, hiyo ni sifa ambayo ni nzito zaidi inayovuta hisia za kuipinga bila lazima ya kusifia huo upande wa pili.
Kiufupi ni kwamba hapo mwanzo nilikupa 'credits' ambazo kumbe huzistahiri kabisa. Pale kwenye "Uwanja wa Chato" nilidhani umeghafirika tu, kumbe ndio kawaida yako.